Na Mwandishi Wetu


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema mawazo ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere akiwa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda aliandika kitabu cha kutetea wanawake ingawa kitabu hicho hakijachapishwa hadi amefariki.

Wasira ameyasema hayo leo Aprili 10, 2026 katika kongamano la kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni Dar es Salaam.

Amesema Mwalimu Nyerere aliandika kitabu cha ‘Uhuru wa Wanawake’ ambacho kilijikita kutetea usawa wa kijinsia, hata hivyo hadi anafariki dunia kilikuwa hakijachapishwa.

Akitoa ufafanuzi huo, amesema sababu ya Mwalimu Nyerere kuandika kitabu hicho ni kutetea wanawake waliokuwa wakiishi familia za Kiafrika zilizoathiriwa na ukosefu wa usawa wa kijinsia.

““Mwalim Nyerere thinking yake ilikuwa ni watu na katika mambo aliyofanya akiwa Makerere ni kuandika kitabu ambacho hakikuchapishwa hadi amefariki kinazungumzia uhuru wa wanawake ambacho kinaitwa Women are not chicken they Egle

“Wanawake wa Tanzania ni mashahidi katika hili kwani, Hayati Mwalimu Nyerere ndani ya kitabu hicho aliibua masuala muhimu na kusisitiza umuhimu wa ushiriki wa wakawake katika uongozi, utawala na maendeleo ya taifa kwa ujumla,” amesema.

Amebainisha kuwa, falsafa kuu ya uongozi wa Mwalimu Nyerere ilijikita katika misingi ya kulinda uhuru wa nchi, kuimarisha umoja wa taifa, kuleta maendeleo ya wananchi na kuendeleza harakati za ukombozi wa Afrika.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...