Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego, amepongeza mchango wa wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo huku akiitaja kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” kuwa nyenzo muhimu ya kuimarisha ustawi wa wakulima na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika jana Singida, Bi. Dendego alisema ujio wa mpango huo kwa mara ya kwanza mkoani humo ni hatua muhimu inayochochea utekelezaji wa malengo ya Serikali ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kimkakati na kuinua kipato cha wakulima.
Hafla hiyo iliwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika, wakulima, pamoja na washiriki wengine katika mnyororo wa thamani wa kilimo. Uongozi wa NBC katika uzinduzi huo uliwakilishwa na Mkuu wa Idara ya Bima, Bw. Benjamini Nkaka, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakulima, Bw. Raymond Urassa, wakiongoza timu ya maofisa wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Kanda ya Kati, Bw Miraji Msuya.
Kwa mujibu wa Bi. Dendego, ujio wa kampeni hiyo unaenda sambamba na jitihada za Serikali ambazo tayari zimeanza kuzaa matunda, ikiwemo usajili wa zaidi ya asilimia 92 ya wakulima mkoani Singida, utoaji wa ruzuku za pembejeo kama mbegu na mbolea, pamoja na uwekezaji katika huduma za ugani na kilimo cha umwagiliaji.
“Kampeni ya NBC Shambani inakuja kuimarisha juhudi hizi kwa kuchochea ujumuishaji wa kifedha kwa wakulima. Hii ni hatua muhimu kuelekea kilimo chenye tija na chenye manufaa kwa wananchi mmoja mmoja, kaya na mkoa kwa ujumla,” alisisitiza.
Aidha, RC Dendego aliwahimiza wakulima kuchangamkia fursa zinazotolewa na kampeni hiyo, akitaja baadhi ya manufaa yake kuwa ni pamoja na akaunti zisizo na makato ya kila mwezi, upatikanaji wa mikopo ya pembejeo na zana za kilimo, elimu ya fedha, pamoja na huduma za bima ya afya na mazao.
Akitoa ufafanuzi kuhusu kampeni hiyo, Bw. Nkaka alisema NBC inaendelea kubuni suluhisho bunifu za kifedha ili kuunga mkono azma ya Serikali ya kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi 10 ifikapo mwaka 2030. Alibainisha kuwa benki hiyo imejikita pia katika utoaji wa elimu ya fedha, huduma za kidijitali, pamoja na bima zinazolenga kupunguza hatari kwa wakulima.
Kwa upande wake, Bw. Urassa alisema kampeni hiyo ya miezo minne, inalenga wakulima wa mazao ya dengu, choroko, mbaazi, soya na ufuta, na inatoa fursa kwa wakulima binafsi pamoja na kupitia vyama vya ushirika kushiriki na kushinda zawadi mbalimbali, ikiwemo pikipiki na kompyuta mpakato (laptops).
“Lengo kuu ni kuwahamasisha wakulima kutumia mifumo rasmi ya kifedha kwa kutunza fedha zao benki. Tunawakaribisha kufungua akaunti za NBC Shambani ili waweze kunufaika na huduma na fursa hizi,” alieleza.
Baadhi ya wakulima walioshiriki uzinduzi huo walieleza matumaini yao juu ya kampeni hiyo, wakihimiza wenzao kuitumia vyema ili kunufaika na fursa za kifedha, elimu, bima na zawadi zinazotolewa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego (wa tatu kulia), akionesha baadhi ya zawadi zinazotolewa kwa washindi kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” inayoratibiwa na Benki ya NBC, yenye lengo la kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya kimkakati ikiwemo dengu, choroko, mbaazi, soya na ufuta mkoani humo. Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ilifanyika jana kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiwemo viongozi wa vyama vya ushirika pamoja na wakulima. Wengine pichani ni Mkuu wa Kanda ya Kati wa NBC, Bw Miraji Msuya (wa tatu kushoto), Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Bw. Benjamini Nkaka (wa pili kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakulima wa NBC, Bw. Raymond Urassa (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Mkoa wa Singida (SIFACU) Bw Julius Kitundu (kulia) na Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Singida Bi Nuria Gulamali (wa pili kulia)

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego (katikati), akipokea zawadi maalum ya picha yake kutoka kwa wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Kanda ya Kati wa NBC, Bw Miraji Msuya (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” inayoratibiwa na Benki ya NBC, yenye lengo la kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya kimkakati ikiwemo dengu, choroko, mbaazi, soya na ufuta mkoani humo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika jana Singida, Bi. Dendego (pichani) alisema ujio wa mpango huo kwa mara ya kwanza mkoani humo ni hatua muhimu inayochochea utekelezaji wa malengo ya Serikali ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kimkakati na kuinua kipato cha wakulima.

Akitoa ufafanuzi kuhusu kampeni hiyo, Bw. Nkaka (pichani) alisema NBC inaendelea kubuni suluhisho bunifu za kifedha ili kuunga mkono azma ya Serikali ya kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi 10 ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wake, Bw. Urassa (pichani) alisema kampeni hiyo ya miezo minne, inalenga wakulima wa mazao ya dengu, choroko, mbaazi, soya na ufuta, na inatoa fursa kwa wakulima binafsi pamoja na kupitia vyama vya ushirika kushiriki na kushinda zawadi mbalimbali, ikiwemo pikipiki na kompyuta mpakato (laptops).

Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Singida Bi Nuria Gulamali akizungumza kwenye hafla hiyo.

Meneja wa Benki ya NBC tawi la Singida Bw David Mushi akizungumza kwenye hafla hiyo.

Baadhi ya maofisa wa NBC wakifafanua kuhusu huduma mablimbali za benki hiyo mahususi kwa wakulima.

Katika hafla hiyo wakulima walipata wasaa wa kusikiliza na kutoa mrejesho kuhusu huduma mbalimbali za benki hiyo.
Hafla hiyo iliwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika, wakulima, pamoja na washiriki wengine katika mnyororo wa thamani wa kilimo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...