Kama sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka kote nchini, Serengeti Apple iliandaa premium brunch experience maalum iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, ikiwapatia wageni waalikwa uzoefu wa kipekee unaoendana na ari ya shamrashamra ya sikukuu.

Likiwa limeandaliwa katika mazingira ya kifahari yenye mandhari tulivu na mpangilio wa kisasa, tukio hilo lilihusisha matukio tofauti kama vile mchanganyiko wa mazungumzo ya karibu, burudani nyepesi ya muziki na huduma ya kiwango cha juu, yote yakikamilishwa na ladha ya kipekee na ya kuburudisha ya Serengeti Apple, kinywaji ambacho kimetengenezwa na kampuni ya Serengeti Breweries hapa nchini Tanzania.

Kuanzia muonekano wa mapambo ya meza mpaka ‘vibes’ za tukio zima kwa ujumla, kila kipengele kilizingatia ubora na umakini, kikitoa taswira halisi ya namna sikukuu na matukio tofauti yanavyoweza kusherehekewa kwa mtindo wa ubora wa hali ya juu.

Kupitia uzoefu huu, Serengeti Apple inaendelea kujenga nafasi yake kama kinywaji kinachoendana na matukio ya kijamii yenye hadhi ya juu, ikiunganisha ladha, mazingira na mtindo wa maisha unaondana na hali ya kisasa.

Mwisho. #serengetiapple #ProudlyTanzanian @serengeti.apple












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...