Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imekutana na Madiwani wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma, na kuwaeleza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji, kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa maji wa miji 28, pamoja na mikakati inayotekelezwa kuboresha huduma hiyo kwa wananchi.
SOUWASA imekutana na Madiwani hao leo Aprili 13, 2026 katika kikao kilichoandaliwa na Mamlaka hiyo, kilicholenga kuwajengea uelewa viongozi hao kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka pamoja na mipango ya muda mfupi na mrefu ya kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama.
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa SOUWASA, Mhandisi Patrick Kibasa, amesema wanaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha huduma ya maji, ikiwemo kuimarisha miundombinu ya uzalishaji na usambazaji pamoja na kupunguza upotevu wa maji.
Ameeleza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana, bado kuna changamoto katika baadhi ya maeneo, na juhudi zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya maji safi na salama kwa uhakika.
Mhandisi Kibasa ameeleza lengo la kuwashirikisha madiwani katika ziara hiyo ni kuongeza uelewa wao kuhusu miradi ya maji ili waweze kusimamia kwa karibu na kuwasilisha kwa usahihi mahitaji na changamoto za wananchi wanaowawakilisha.
Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya SOUWASA na viongozi wa wananchi ni muhimu katika kuhakikisha mipango na miradi ya maji inatekelezwa kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya kwa jamii.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Abraham Egno Mbunda, amesisitiza umuhimu wa kudumisha ushirikiano na mawasiliano ya karibu kati ya madiwani na menejimenti ya SOUWASA ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Amesema ziara za viongozi kwenye miradi ya maendeleo ni muhimu kwa kuwa zinawapa uelewa wa moja kwa moja kuhusu utekelezaji wake na kusaidia kufanya maamuzi sahihi.
Baadhi ya madiwani wameeleza kuwa ziara hiyo imewapa uelewa mpana kuhusu mradi wa Miji 28, na matarajio, ni kuona mradi unakamilika na kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji, hususan katika maeneo ya pembezoni.
Kwa ujumla, Mradi wa maji wa miji 28 ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuboresha huduma ya maji katika maeneo ya mijini, na unatarajiwa kuchangia kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wakazi wa Manispaa ya Songea.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...