Na.Ashura Mohamed -Arusha

Taasisi kongwe ya dini ya kiislamu ya Twariqa Tulqadirya Arazakia Jailania Tanzania yenye makao yake makuu mkoani Arusha, imedhamiria kufanya sensa ya watu  na mali za taasisi hiyo ili kupata Idadi sahihi ya waumini wake.

Lengo la  zoezi hilo ni kuweza kufanya kazi kwa Ufanisi na kuyafahamu makundi  mbali mbali yaliyomo katika taasisi hiyo yakiwemo  makundi ya Viongozi Vijana,Wanawake,Walemavu,Yatima,Wajane na Wagane ili waweze kupatiwa huduma stahiki katika Mikoa yote ya Tanzania .

Akizungumza na Vyombo vya Habari mkoani Arusha Mwenyekiti wa Twariqa Taifa Shekhe  Mubaraka Salim Gahran amesema kuwa taasisi hiyo  ilifanya sensa ya kitwariqa  mnamo mwaka 1932,ambapo imepita kipindi kirefu bila zoezi hilo kufanyika hali ambayo inapelekea tasisi kushindwa kuwa na Idadi kamili ya watu  pamoja na mali zilizopo sasa.

Shekhe  Gahrani amesema kuwa  pia Ofisi yake imeona  ni vema kufanya uhakiki wa mali zilizopp kwa kuwa tangu kiongozi wao  Daruweshi Mti Mkavu alipofariki takribani mwaka mmoja na nusu  kuna baadhi ya vitu wanapaswa kuviweka sawa ili kuhakiki mali zote na kuepusha migogoro isiyo ya lazima ndani yao ikiwa ni pamoja na watu binafsi kujimilikisha mali za taasisi hiyo nchini.

"Hii ni sensa ya kawaida ya kitwariqa na inawahusu wanatwariqa wa Daraweshi Mti Mkavu na tunataka kuhakiki  kila kitu kuanzia Idadi ya Waridi wetu waliopata Ijaza,Elimu zao za kawaida,kufahamu haya yote itatuwezesha sisi  Viongozi kujua mahitaji yao na tuna watu wa aina gani na tunawahudumiaje na kwa namna gani bila kusahau migogoro isiyo ya lazima  na isielewele vinginevyo.Alisisitiza Shekhe Gahran 

Nae katibu mkuu wa twariqa Taifa shekhe  Haruna Hussein Lotha ameiomba serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwapa Ushirikiano wakati wa zoezi hilo ili kufanya zoezi hilo kutekelezwa kwa utulivu na kwa kufuata taratibu.

Shekhe Haruna Hussein amesema kuwa tangu wameingia madarakani hawajui idadi ya waumini wao,majengo wala mali walizonazo ili kuwasaidia kujua mapungufu yaliyopo na kisha kuboresha kwa kuwa kazi ya dini ni kujenga Imani za watu na kuwahudumia kiroho.

"Taasisi  yetu imekuwa ikishirikiana  na serikali yetu kila eneo hivyo tunatazamia kuwa mashirikiano haya  yatakuwa endelevu na  pia tumetumia vyombo vya habari ni kuhakikisha jamii inaendelea  kupata taarifa kwa wakati na zoezi litakapoanza katika mikoa yote ya Tanzania,liwe rahisi "Amesisitiza Katibu Lotha.

Pichani ni Viongozi wa Makundi Mbali mbali wa Taasisi ya TWARIQA TULQADIRIYA JAILANIA TANZANIA wakiongizwa na Mwenyekiti wake Taifa Shekhe Mubarak Salim Gahran na Katibu Mkuu Taifa Sheikh Haruna Hussein  mara baada ya kumaliza kikao Cha ndani.
Mwenyekiti wa TWARIQA Taifa Shekhe Mubarak Salim Gahran wa Pili kulia akiwa na Viongozi Wengine wakati wakizungumza na Vyombo vya Habari


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...