Taasisi ya Saratani Ocean Road imeendelea kutoa elimu na huduma za uchunguzi wa saratani mbali mbali katika Maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa 2026.

Kilele cha maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Zimbwini, Kibiti Mkoa wa Pwani, ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, ambayo ni maaluku kwa chanjo, Bima Afya kwa wote na usafi wa mazingira.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Meneja wa Huduma za Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma, DK. Maguha Stephano, amesema taasisi hiyo inaunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha  wananchi wanapata elimu kuhusu saratani.

Maguha amesema pia wanahakikisha wananchi wanapata chanjo zinazozuia maambukizi ya virus I vinavyosababisha saratani za mlango wa kizazi, saratani ya  ini na huduma za uchunguzi wa saratani mbali mbali, zikiwemo mlango wa kizazi, matiti na tezi Dume kwa wanaume.

Amesema Saratani ya tezi Dume inafanyika kwa njia ya kipimo cha damu na huduma hizo zinatolewa bila malipo na taasisi hiyo.

Aidha Maguha amewaomba wananchi wa Mkoa wa Pwani katika katika Wilaya ya Kibiti kutumia fursa hiyo  kupata huduma hizo bure.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...