Na Byera Deus,Bukoba 

Kutokana na Mabadiliko ya bei elekezi ya mafuta iliyoanza kutumika Aprili Mosi mwaka huu  Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wamekutana na wadau wanaotumia Usafiri wa majini   kufanya   tathmini ya athari za bei ya mafuta na  kujadili uwezekano wa kurekebisha au kuongeza nauli za abiria katika njia mbalimbali za usafiri majini

Afisa Uhusiano wa TASAC Kanda ya Ziwa, Said Mkabakuli, alisema lengo la shirika hilo ni kulinda maslahi ya wananchi pamoja na watoa huduma kwa kuhakikisha kunakuwa na uwiano sawa  katika mabadiliko ya nauli, ili wananchi waweze kuendana na gharama bila kubebeshwa mzigo mkubwa, 

Alisema kuwa  maoni ya wadau wanaotumia vyombo vya majini  kuhusu athari za Ongezeko la bei ya mafuta  yaapaswa kutolewa na kupokelewa bila  kuathiri huku huduma bora zinazotolewa kwa wananchi wanaotoka eneo moja kwenda eneo lingine

"Changamoto mafuta kupanda linapotokea linaathiri pande zote mbili ninachoweza kusema ni kuwa tutoe maoni bila kuegemea upande kwa sababu kama wamiliki vya vyombo vinavyotoa huduma na kusafirisha wateja Vitoe huduma bila kumuumiza sana mwananchi gharama itakayoongezeka isiwe kubwa sana ya kukwamisha huduma"alisema Mkabakuri 

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji, Issaya Tendega, alisema Serikali itahakikisha maoni yote yanayokusanywa yanawasilishwa katika mamlaka husika na kufanyiwa kazi kwa wakati, huku akisisitiza kuwa majibu yatarejeshwa kwa wadau kabla ya Aprili 26, 2026 ili kuwezesha maamuzi sahihi.

Alisema kuwa ni vyema mamulaka zikaendelea kufatilia kwa ukaribu ili  bei ya mafuta ikipungua gharama za usafirishaji wa abiria zisiendelee kuwa juu Bali zishuke pia   wananchi wapunguziwe mzigo.

"Tuna huduma nyingi sana zinazoenda visiwani na wananchi wetu wengi na watumishi wanaoishu huko, ni kweli bei ya mafuta Iko juu na athari zimeanza Kujitokeza kama mahitaji ya msingi kupanda ,Hapa inabidi maridhiano kati ya wananchi na wamiliki vya Usafiri majini kwa kuzingatia matakwa halisi ya mamulaka husika ,tunaomba ukaribu huo uendelee siku mafuta ya kushuka basi na wananchi wetu   bei za kwenda visiwani zishuke"alisema Tendega

Kwa upande wa wadau, baadhi yao akiwemo Mwalimu Ivona Bajumuzi, wameipongeza TASAC kwa kuwashirikisha wananchi katika mchakato huo, wakieleza kuwa hatua hiyo inasaidia kuongeza uelewa pale ambapo mabadiliko ya nauli yanapotokea.

Hata hivyo, baadhi ya wadau walioudhuria mkutano huo  wameeleza hofu juu ya ongezeko la nauli kubwa za pambeni ambazo wamiliki wanaweza kujiongezea bila kufuata utaratibu , wakitaka kuwepo kwa suluhisho litakalopunguza gharama  na mamulaka kuweka Ukomo  wa nauli zitakazopangwa bila kuathiri maisha ya watumiaji wa Usafiri wa majini wa Kila siku. 






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...