GEITA VIJIJINI: ZAIDI ya wananchi 700,000 kutoka kata 19 katika Mkoa wa Geita wanatarijiwa kunufaika na mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya Sh bilioni 124 katika utekelezaji wake.
Mradi huo unatarajiwa kuanza kufanya kazi Septemba 30 mwaka huu na kuzalisha jumla ya lita milioni 45 za maji kwa siku.
Hayo yalibainishwa leo Aprili 16,2026 na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (GEUWASA), Mhandisi Frank Changawa mbele ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi alipokagua utekelezaji wa mradi huo uliopo katika Kata ya Senga Geita Vijijini mkoani Geita.
Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Kihongosi amesema huo ni miongoni mwa miradi ya miji 28 ambayo inatekelezwa nchi nzima na unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa upatikanaji wa maji safi na salama kwa ufanisi na kwa muda mrefu.
Amesema katika ilani ya Uchaguzi iliyopita, serikali iliahidi kuhakikisha huduma ya maji mijini inafikia asilimia 95 na vijijini asilimia 85, lakini mradi huo utakapokamilika, watavuka lengo hilo na kufikia upatikanaji wa maji kwa asilimia 100.
“Kwa kweli nikawa naona maajabu mengi, tumekagua miradi mingi, lakini huu ni mmoja wa miradi mikubwa sana. Hongereni sana, niwapongeze viongozi, wataalamu na wasimamizi wa mradi kwa weledi wao, mmeonesha umiliki mkubwa wa kitaaluma na kuhakikisha kazi inafanyika kwa ufanisi,” amesema Kihongosi.
Awali, akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (GEUWASA), Mhandisi Frank Changawa amesema gharama ya mradi huo ni dola milioni 53.463, na hadi sasa utekelezaji umefikia asilimia 80 ya kazi nzima ya ujenzi na miundombinu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...