Na Farida Mangube, Morogoro

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limewakamata watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya mauaji yaliyotokea katika wilaya za Malinyi, Kilombero na Kilosa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi wa polisi ACP Andrew Gabriel Kantimbo amesema tukio la kwanza lilitokea katika kijiji cha Nyameni, kata ya Ulaya wilayani Kilosa, ambapo mwanamke aitwaye Janeth Ernest Mazengo (52) alifariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa na mumewe, Amos Zakaria Kisomeko (64).

 Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mtuhumiwa alimshambulia marehemu kwa muda mrefu na kumsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake.

Katika tukio jingine lililotokea wilayani Kilombero ambapo Ramadhani Sadick Joseph (35) anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua Messe Germanus Ngayungwa (23) mkazi wa Ifakara,  marehemu alidaiwa kupigwa na kitu kizito hadi kupoteza maisha, huku chanzo kikitajwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa upelelezi wa matukio hayo unaendelea, na watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kufuata taratibu za kisheria pale wanapokumbana na migogoro, ili kuepuka matukio ya ukatili yanayoweza kusababisha vifo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...