NA DIANA BYERA DEUS-KARAGWE.

Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Karagwe, Mkoani Kagera, Wandera Rwakatare, ametoa wito kwa wawekezaji wa shule binafsi kupunguza vita ya kuchonganishana na kuzua taarifa za taharuki, badala yake wajikite kutoa elimu bora yenye ushindani ili kupata wanafunzi wengi.

Kupitia mahafari ya 14 ya kidato cha sita ambayo yalifanyika katika shule ya Ushirika wa wakulima wa kahawa Karagwe na Kyerwa KDCU alisema kuwa amekuwa akisikitishwa na taarifa za sasa za kuvumisha ambazo zinaleta taharuki na taarifa hizo utolewa mara baada ya kuona shule inafanya vizuri bila kwenda kujifunza shule hiyo inatumia mbinu gani kujifunza.

Alisema ni vyema wawekezaji wa maswala ya elimu watambue kuwa elimu inayovutia ni ile inayoleta nidhamu wa watoto, ushindi, mazingira bora ya kujifunzia, uelewa wa viwango kwa watoto, na sio taarifa za kijipanga kusambaza uongo ambapo amedai kuwa wanavumisha taarifa za uongo na uvumishi huo hawatavumiliwa.

“Nyaishozi Sekondari kwa miaka 6 Mfululizo imekuwa ikitokea nafasi za juu kitaifa katika mitihani ya kidato cha sita cha pili na cha nne ,na kutokana na ubora huo kumekuwa kuna taarifa mbaya ambazo mwanzoni zilituweka katika wasiwasi ila baada ya uchunguzi tumegundua kuwa ni vita ya kuharibiana ili kupata watoto ,sasa muda wa kufanya hiyo michezo utumike kuboresha shule na kupanga njia mpya za kuongeza maharifa kwa watoto”.

Alisema ili kudhuitisha taarifa hizo alileta watoto kadhaa kusoma hapo ili kubaini yanayosemwa lakini ghafla hata watoto hao ambao hawakuwa na uelewa sana waligeuka lulu na kushinda na hawakuishia kushinda mienendo na tabia zao zilibadilika kuwa njema zaidi jambo ambalo lilimvuatia pia kuhamisha mtoto wake Shinyanga na kumleta shuleni hapo ,ambapo ametoa nasaha ya wawekezaji kupendana na kushindana kukuza elimu ili kuvutia wazazi.

Alipongeza shule hiyo kwa namna inavyohakikisha watoto wengi wa wakulima wanaotoka wilaya za Karagwe na Kyerwa wanavyopata elimu bora na kusoma hadi elimu ya juu kwa lengo la kurudi kubadilisha jamii na kueneza kilimo cha sayansi kinachoendana na mabadiliko ya sasa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Audax Gereon alisema kuwa shule hiyo unaendelea kutiiza matakwa yake ya kutoa elimu bora kwa watoto wa wakulima na watoto wote ambapo alisema kuwa kwa sasa shule hiyo inapokea watoto wote kutoka mikoa ya Tanzania.

Alisema kuwa kwa wale watoto ambao wazazi wao ni wakulima wa kahawa wanaendelea kukatwa kidogo kidogo kwenye kahawa na watoto wao wakisoma bila kubuguziwa wala kuhojiwa.

Alisema shule hiyo miaka 6 Mfululizo haijapata daraja la tatu wala la nne inapata daraja la kwanza na la pili na sasa uongozi wa shule hiyo na wanafunzi wamekubariana kupata daraja la kwanza pekee,huku akihaidi kuwa maadili na nidhamu ni kipaumbele cha kwanza katika shule hiyo ili kuleta matokeo mazuri.

Baadhi ya wazazi walipogeza elimu inayotolewa shuleni hapo huku wakidai kuwa watoto hao wanapokuwa katika mapumziko wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa elimu ya kilimo cha kahawa katika familia zao na waliowazunguka kwani somo la kilimo katika shule hiyo ni la wote na halina ubaguzi.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...