Kampuni ya Mawasiliano Yas kwa kushirikiana na Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania, imefanya kambi maalum ya huduma za matibabu ya macho iliyowahudumia zaidi ya wakazi 4,000 katika Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Ushirikiano huo unaakisi dhamira ya Yas katika kuwekeza kwenye ustawi wa jamii, sambamba na jitihada za kuboresha afya ya macho na kupunguza matatizo ya uoni yanayowakabili wakazi wa maeneo ya vijijini wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Akifungua kambi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, aliipongeza Yas na Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania katika kufanikisha zoezi hilo, akibainisha kuwa matatizo ya macho bado ni changamoto kubwa katika jamii.
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kunufaika na huduma hizo za bure, akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi za kijamii una mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya nchini.
Mratibu wa kambi hiyo, Ain Sharif, alisema huduma hizo za bure zinajumuisha uchunguzi wa macho, utoaji wa dawa na miwani kwa waliokutwa na tatizo, ushauri wa kitaalamu pamoja na upasuaji mdogo wa mtoto wa jicho kwa wagonjwa watakaobainika kuwa na tatizo hilo.
Aliongeza kuwa wagonjwa watakaohitaji matibabu ya juu zaidi watapewa rufaa ili waweze kuendelea kupatiwa huduma katika vituo vya afya vyenye uwezo mkubwa, huku kipaumbele kikitolewa kwa watoto ili kuwawezesha kurejea masomoni bila changamoto za uoni.
“Lengo la kambi hii ni kuwafikia wananchi wengi ambao hawana uwezo wa kupata matibabu ya macho. Tunatarajia kuhudumia zaidi ya watu 4,000 ndani ya siku hizi tatu, na tayari timu ya madaktari bingwa na wauguzi imewasili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ufanisi,” alisema Sharif.
Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa Yas Mkoa wa Singida, Bw. Emmanuel Kaminyonge, alisema ushiriki wa Yas katika zoezi hilo, ni sehemu ya dhamira yake ya kuendelea kuwa karibu na jamii na kuchangia maendeleo ya kijamii nje ya huduma za mawasiliano.
“Yas tunaamini afya bora ni msingi wa maendeleo ya jamii. Kupitia ushirikiano huu, tunalenga kusaidia kuboresha maisha ya wananchi wa Iramba na maeneo jirani kwa kuwapatia huduma muhimu za afya ya macho bila gharama,” alisema Kaminyonge.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, akiongoza zoezi la uchunguzi wa macho katika kambi ya matibabu ya macho bure iliyofanyika hivi karibuni katika Wilaya ya Iramba. Zoezi hilo liliandaliwa na Yas kwa kushirikiana na Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania. Huduma iliwafikia zaidi ya wakazi 4,000, ikichochea juhudi za upatikanaji wa huduma muhimu za afya ya macho kwa jamii zilizo pembezoni.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...