Muungano wa watoa huduma za mawasiliano nchini (Telco Operators Consortium) umekamilisha rasmi ujenzi wa minara ya mawasiliano 758 na kukabidhi zaidi ya kilomita 1,100 za miundombinu ya nyaya za fiber optic kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatua ambayo ni mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mpango wa taifa wa kupanua miundombinu ya mawasiliano.

Hafla ya makabidhiano imefanyika katika kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mradi huo umejengwa kupitia ushirikiano wa muda mrefu kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP), ukiwa na lengo la kuharakisha upatikanaji wa intaneti ya kasi na kuimarisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB).

Kwa mujibu wa muungano huo, mradi huo unahusisha njia kuu za fiber optic katika korido za Dodoma–Mwanza, Morogoro–Ifakara na Moshi–Rombo, zenye urefu wa takriban kilomita 1,193.

Pia unajumuisha miundombinu ya fiber ya mijini katika miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Mwanza, Tanga, Moshi, Morogoro, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Biharamulo, Makambako na Musoma. Sehemu nyingine za mradi bado ziko katika hatua za ujenzi na zitakabidhiwa baada ya kukamilika.

Rais Samia Suluhu Hassan ameupongeza muungano huo kwa mchango wake katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kidijitali nchini na kuongeza ushindani wa kiuchumi kupitia miundombinu bora ya mawasiliano.

Akizungumza wakati wa halfa kwa niaba ya muungano huo, Mwenyekiti wa Muungano Bw. Pierre Canton Bacara ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, amesema mradi huo unaonesha umuhimu wa ushirikiano endelevu kati ya Serikali na sekta binafsi katika kufanikisha malengo ya kitaifa ya uimarishaji wa mawasiliano.

Aliongeza kuwa miundombinu hiyo itaongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali na kuchochea ukuaji wa sekta muhimu ikiwemo huduma za kifedha, biashara mtandao (e-commerce), afya na elimu kupitia mawasiliano yaliyoimarishwa.

Kwa upande wa Kampuni ya Mawasiliano ya Yas, imekuwa na jukumu kubwa la kiutendaji ndani ya muungano huo, ikishiriki katika ujenzi na usambazaji wa mtandao katika maeneo mbalimbali nchini.

Kampuni hiyo imechangia takriban asilimia 33 ya maeneo yote yaliyokamilishwa (saiti 261) na pia imeboresha mtandao wake kote nchini kutoka 2G na kuwa 4G kama sehemu ya mpango wa kisasa wa miundombinu ya mawasiliano.

Aidha, Yas Tanzania imewekeza zaidi ya TZS trilioni 1 katika miundombinu ya mtandao na kwa sasa inaendesha mojawapo ya mitandao mikubwa zaidi ya 4G na 5G nchini, inayofikia zaidi ya asilimia 95 ya wananchi.

Kampuni hiyo imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kupanua huduma jumuishi za mawasiliano hadi maeneo ya vijijini na maeneo ambayo bado hayajafikiwa kikamilifu.

“Kadiri Tanzania inavyoendelea kuelekea kuwa kitovu cha kidijitali cha ukanda wa Afrika Mashariki, ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi utaendelea kuwa nguzo muhimu ya kuharakisha mageuzi haya,” alisema.

 Mwenyekiti wa muungano huo.Muungano huo pia umeeleza kuwa uungwaji mkono wa kisera, ikiwemo mapitio ya gharama za intaneti, utaongeza ushindani wa Tanzania kama kitovu cha mawasiliano kikanda na kusaidia ongezeko la matumizi ya data nchini.

Makabidhiano haya ya miundombinu, yanayojumuisha minara ya mawasiliano na Mkongo wa Taifa wa fiber optic, na ni sehemu ya ajenda pana ya mageuzi ya kidijitali Tanzania, chini ya Ajenda 2050, yenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa mawasiliano ya bei nafuu, uhakika na imara kote nchini.-





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...