Zaidi ya Watalii 90 wametembela Hifadhi ya Taifa Mkomazi kuvinjari na kufurahia utalii wa ndani leo Aprili 11, 2026 kufuatia ufunguzi wa tamasha la utalii lijulikanalo kama Same Utalii Festival msimu wa Tatu katika viwanja vya stendi wilayani Same, Mkoani Kilimanjaro.

Watalii hao walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi ikiwemo Mbula, Kisima na Njiro na kujionea wanyamapori aina ya faru weusi, kivutio kinachowavutia wazawa na wageni lukuki toka nje na ndani ya mipaka ya Same kushuhudia ikolojia ya wanyama hao.

Akizindua rasmi tamasha hilo Waziri Mkuu (Mst.) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyelitumikia Taifa kwa kipindi cha Awamu ya Nne kati ya mwaka 1990 hadi 1994 Mhe. John Malecela alisema kuwa matamasha haya ni kichocheo kikubwa cha utalii na hifadhi pia zina nafasi kubwa ya kuibua mazao mapya ya utalii yatakayochagiza kuongeza idadi ya watalii  kutembelea hii kwa kuwa na vionyo tofauti.

Aidha, Mhe. Malecela aliongeza kuwa utalii wetu uanze na sisi watanzania wenyewe ndani ya vivutio vyetu na hii ni kutokana na gharama nafuu zilizowekwa pamoja na uwezo mkubwa wa kufikia maeneo hayo kwa wepesi tofauti na wale wanaotoka maeneo ya mbali.

Naye, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. John Mabula alieleza kuwa idadi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi imeongeza kwa kiasi kikubwa kutoka 7800 kwa mwaka na kufikia 11000 kwa mwaka 2022 hadi 2026. Kadhalika alieleza kuwa uwepo wa vivutio na ongezeko la wageni ni fursa kwa wazawa kuweza kujiinua kibiashara na kuongeza kipato katika kaya zao.

Kwa, upande wake Mkuu Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni alieleza kuwa Hifadhi ya Taifa Mkomazi iwape fursa vijana wa bodaboda kwa kutoa elimu ya kuongoza wageni ili wanapowapokea watalii waweze kuwakaribisha na kuwapa miongozo ya awali itakayochangia pato katika majukumu yao.

Hifadhi ya Taifa Mkomazi imekuwa moja ya kivutio pendwa katika  tamasha hili kwa kuwakutanisha wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya wilaya ya Same kutembelea wanyamapori adimu ikiwemo faru weusi, mbwa mwitu pamoja na uoto wa asili unaoipamba hifadhi hiyo. 













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...