Na Janeth Raphael MichuziTv-Bungeni Dodoma
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan kwa hatua mbalimbali za maendeleo zilizotekelezwa katika Mkoa wa Kigoma, akisema zimekuwa faraja kubwa kwa wananchi waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za muda mrefu za miundombinu.
Mbunge huyo pia alimpongeza Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega kwa juhudi zake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya ujenzi na maboresho ya barabara nchini.
Akichangia hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2026/27 leo Mei 21, 2026, bungeni jijini Dodoma, Baba Levo alisema wananchi wa Kigoma Mjini wamepitia mateso makubwa kwa muda mrefu kutokana na changamoto za miundombinu, lakini sasa wameanza kuona matumaini kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali.
Amesema maendeleo yanayoendelea kufanyika Kigoma yamefuta machozi ya wananchi wengi ambao kwa miaka mingi walikuwa wakihitaji maboresho ya barabara na huduma nyingine muhimu za usafiri.
“Wananchi wa Kigoma Mjini wameteseka sana kwa muda mrefu, lakini leo hii serikali imefuta machozi yao kutokana na kazi kubwa inayofanyika. Tunamshukuru Rais Samia pamoja na Waziri Ulega kwa kusikiliza kilio cha wananchi,” alisema Baba Levo.
Katika mchango wake, mbunge huyo pia alimuomba Waziri Ulega kuyachukua maoni na changamoto zilizotolewa na wabunge mbalimbali kama sehemu ya kuongeza kasi ya utatuzi wa kero za wananchi.
Aidha, Baba Levo aliendelea kuishauri Wizara ya Ujenzi kuangalia uwezekano wa kujenga daraja la juu (flyover) katika moja ya maeneo hatarishi ya Kigoma Mjini ambako wananchi wamekuwa wakigongwa mara kwa mara kutokana na msongamano na changamoto za miundombinu ya barabara.
“Naomba nipate heshima ya kuwa na barabara za juu Kigoma Mjini. Tumeomba daraja kama lile la Manzese kwa sababu kuna eneo wananchi wanagongwa sana, hivyo tunahitaji suluhisho la kudumu,” alisema.
Kauli hiyo imeibua mjadala bungeni huku wabunge wengine wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya kisasa ili kuimarisha usalama wa wananchi na kukuza uchumi wa maeneo mbalimbali nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...