WANANCHI wa manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamelalamikia gharama za nauli za bajaji zinazofanya ruti zake kama daladala ndani ya manispaa hiyo na kuiomba Serikali kuingilia kati kunusuru adha hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamedai kuwa hapo awali walikuwa wakitozwa nauli ya 700 lakini kwa sasa wanatozwa 1,000- 1500 hali ambayo imegeuka kuwa adha kwao na kuwafanya wengi kushindwa kumudu gharama

Mmoja wa wananchi hao, Amina Salimu mkazi wa Soweto amesema kuwa, kwa sasa wamekuwa wakilazimika kutembea kwa miguu kutoka mjini Moshi kwenda na kurudi Soweto kutokana na kushindwa kuimili gharama za nauli.

"Mwanzoni tulikuwa tunatumia 1400 kwenda na kurudi Soweto lakini kwa sasa imeongezeka mpaka kufikia 2,000 hadi 3000 hii ni gharama ya kutuumiza sisi wananchi tunaiomba serikali kuingilia kati kutunusuru wananchi" alisema Amina.

Naye Rukia Juma ambaye ni mama lishe na mkazi wa Msaranga alisema kuwa kwa sasa ameanza kushindwa kumudu gharama za kuendesha familia kwani amekuwa akilipwa 4000 kwa siku lakini analazimika kutumia 3000 kwa ajili ya nauli hali ambayo imelekea kushindwa kumudu kutunza familia.

Mwananchi mwingine, Christofa Lyimo alisema kuwa, kwa sasa wamekuwa wakishindwa kwenda hospitali ya KCMC kuwaangalia na kuwahudumia wagonjwa wao ambao wamelazwa katika hospitali hiyo kutokana na gharama za usafiri kupanda.

Akijibu malalamiko hayo, Meneja wa mamlaka ya uthibiti wa usafiri ardhini (LATRA)mkoa wa Kilimanjaro, Paul Nyello alisema kuwa, Sheria ya LATRA haifanyi udhibiti wa tozo za bajaji na ni makubaliano ya abiria na mtoa huduma.

Alisema kuwa kwa sasa wapo katika mchakato wa kuongeza mabasi njia za mjini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...