NA MWANDISHI WETU

 BARAZA la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi (CCM) limeeleza kuridhishwa na utekelezaji wa   miradi inayotekelelezwa  kwa   ubia baina ya Chama, jumuiya zake na wadau .

Hayo yameelezwa na wajumbe wa baraza hilo katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo  mkoani Dar es salaam leo,  inayotekelezwa na CCM,  Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) .

Akizungumza baada ya ziara  hiyo ,Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini  la CCM, Vuai Ali Vua,  amesema   CCM ni  Chama cha siasa   kinacho taka kujitegemea  hivyo   ili kufikia azama hiyo  kinafanya shughuli za kisiasa na kiuchumi.

"Hivyo  wito kwa watendaji wetu wa Chama  kuanzia  ngazi za shina, tawi kata, wilaya mkoa na taifa  ni kutumia fursa zilizopo katika taifa letu kupromoti  miradi ya CCM kuongeza pato la Chama,"alisema Vuai.

 Ameeleza  ni wajibu wa watendaji wa CCM  na jumuiya zake kuwa wabunifu  wa kiuchumi na kisiasa  kwani ndiyo aina ya watendaji ambao chama kintegemea kuwa nao  katika kipindi hiki.

Akizungumzia a mradi wa jengo la kitega uchumi la  Jumiuya ya Wazazi Tanzania katika eneo la Ilala Mchikichini  Kiwanja 2C na 2B wenye thamani  ya sh. bilioni 2.3, Vuai  amesema baraza limeridhishwa na utekelezaji wa mradi huo  ambao umesuasua kwa miaka mingi sasa.

Ameshauri Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi  Tanzania, Ally  Hapi,  kukaa na Kampuni ya MCL ambaye ni mwekezaji wa mradi huo  wa ghorofa  moja unaohusisha , nyumba za makazi na ofisi  kuongeza  ghorofa zaidi kutoka ghorofa moja iliyopo.

Awali Mjumbe wa Bodi hiyo, Kapten mstaafu John Chiligati, alishauri  kwa kuwa mradi huo ulikusudiwa kujenga ghorofa 20 ambapo msingi wake  unaweza kubeba ghorofa hizo  ni vyema utekelezaji ukaendelea.

Pia, Mjumbe wa Bodi hiyo, Andrew Chenge, ameshauri  Jumuiya ya Wazazi kukaa vyema na wawekezaji   Kampuni ya MCL  kuhakikisha uwekezaji huo unakuwa endelevu na haushii hapo ili ulete tija zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania,  Fadhili Maganya, amesema  kukamilika kwa jengo hilo kumechukua muda mrefu kutokana na migogoro 'mazonge'  mbalimbali  ambayo hata hivyo ilitatuliwa na utekelezaji kufanyika hatimaye jengo kukamilika.

Katibu wa Jumuiya hiyo,  Ally Hapi, amesema amepokea ushauri na maelekezo ya baraza hilo hususan kukaa na Kampuni ya Uwekezaji ya MCL kwaajili ya kuendeleza ujenzi  wa jengo hilo   kujengwa kwa zaidi ya  ghorofa moja .

Bodi hiyo pia ilikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la kitega uchumi la UWT  linalojengwa  katika eneo  la SUWATA, jijini Dar es Salaam kwa gharama ya sh. bilioni 6  na kupongeza umoja huo  kwa hatua hiyo kubwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...