Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba jana Mei 11, 2026 alishiriki chakula cha jioni cha kitaifa kilichoandaliwa na Rais wa Kenya Dkt. William Ruto kwa heshima ya Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na Ufaransa
Dkt. Mwigulu yupo nchini Kenya akimuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na Ufaransa (Africa Forward: Africa–France Partnership for Innovation and Growth Summit) unaofanyika jijini Nairobi, Kenya.
Lengo la mkutano huo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, teknolojia, nishati, afya, Akili Unde (AI), kilimo, uchumi wa buluu pamoja na viwanda.
WAZIRI MKUU, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, Mheshimiwa Emmanuel Macron, Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt. William Samoei Ruto pamoja na Mke wa Rais wa Kenya, Mama Rachel Ruto, wakati wa chakula cha jioni cha kitaifa kilichoandaliwa kwa heshima ya Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki Mkutano wa Ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa (Africa Forward Summit: Africa–France Partnership for Innovation and Growth) unaofanyika jijini Nairobi, Kenya.






.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...