Jamii imetakiwa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu na badala yake kuwapa nafasi sawa katika shughuli za kijamii na kiuchumi ili waweze kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
Wito huo umetolewa na Afisa Mradi wa Tuinuke Pamoja chini ya Shirika la Aga khan foundation kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, kutoka Wilaya za Chamwino na Dodoma, Bi Agnes Nkuba, wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku nne yaliyowakutanisha vikundi mbalimbali vya watu wenye na wasio na ulemavu jijini Dodoma.
Amesema watu wenye ulemavu wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi kama watu wengine endapo watapatiwa mazingira rafiki, ushirikiano na maelekezo sahihi ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali, amesema kupitia mradi wa Tuinuke Pamoja wameweza kushirikiana nao kwa karibu na kujionea uwezo wao mkubwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo bila kikwazo chochote.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Walemavu kutoka Tarafa ya Mwitikila Wilaya ya Bahi, Amos Madeha Ndolee, amesema hapo awali walikosa uelewa wa namna ya kujikwamua kiuchumi, hata hivyo, kupitia Shirika la Aga Khan Foundation na mradi wa Tuinuke Pamoja, wamewezeshwa na sasa wanajipatia kipato kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Aidha, ameiomba serikali kuanzia ngazi za vijiji kuwabaini watu wenye ulemavu na kuwasaidia ili waweze kupata fursa za maendeleo kama wananchi wengine, pia amelishukuru Shirika la Aga Khan Foundation kwa kufika vijijini na kutoa msaada pamoja na elimu muhimu kwa vikundi vyao.
Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo wameeleza kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuboresha utendaji wa vikundi vyao, hususan katika kuandaa taarifa sahihi za mapato na matumizi, kupata elimu ya kijinsia na kuwajengea uwezo wa kufikiri kimaendeleo.
Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku nne mfululizo jijini Dodoma yakihusisha wanavikundi 17 kutoka Wilaya za Bahi, Chamwino na Dodoma, ikiwemo vikundi vipya nane vya watu wenye ulemavu, Lengo la mafunzo hayo likiwa ni kuwajengea washiriki uelewa wa pamoja kuhusu mradi wa Tuinuke Pamoja, elimu ya masuala ya kijinsia, elimu ya fedha pamoja na ufuatiliaji na tathmini wa shughuli za maendeleo.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...