Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Yahya Ramadhan Kido amesema Mkoa wa Kagera unaendelea kufanya vizuri katika uzalishaji wa zao la kahawa, huku akibainisha kuwa hadi sasa mkoa huo una jumla ya miche ya kahawa milioni 85 inayotarajiwa kuongeza tija na kuinua uchumi wa wakulima.
Kanali Kido amesema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa kahawa mkoani Kagera, ambapo ameeleza kuwa Serikali kupitia ushirikiano na wadau mbalimbali imeendelea kusambaza miche ya kahawa kwa wananchi, huku miche milioni 36.75 ikiwa tayari imetolewa kwa wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo muhimu la biashara.
Amesema katika msimu wa 2025/2026 pekee, miche milioni 13.7 ilisambazwa kwa wakulima kupitia ushirikiano kati ya Bodi ya Kahawa Tanzania, halmashauri, vikundi vya wakulima pamoja na sekta binafsi.
Aidha, ameitaka Bodi ya Kahawa Tanzania kuendelea kusambaza miche zaidi kwa wakulima pamoja na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo, hususan wadudu waharibifu aina ya bungua mweusi ambao wamekuwa wakisababisha hasara kwa baadhi ya wakulima.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania, Primus Kimaryo amesema bado kuna haja kubwa ya kuendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafanyabiashara wa zao hilo ili kudhibiti biashara ya kahawa inayofanyika kwa njia za magendo.
Amesema baadhi ya watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wanatoka ndani ya jamii husika, hali inayochangia upotevu wa mapato kwa wakulima pamoja na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Primus Kimaryo amewataka wafanyabiashara kuachana na vitendo vya kuuza kahawa kwa njia zisizo rasmi, huku akiwataka wakulima kuwa waaminifu kwa kuuza kahawa kupitia mifumo halali ili waweze kunufaika zaidi kiuchumi.
Katika hatua nyingine, amesema Mkoa wa Kagera umeendelea kufanya vizuri katika uzalishaji wa kahawa, ambapo uzalishaji wa kahawa ya maganda umefikia zaidi ya tani elfu 50, hatua inayodhihirisha ukuaji wa sekta hiyo ndani ya mkoa huo.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...