Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Kenya imetoa hati rasmi za vyuo vikuu kwa Kenya Advanced Institute of Science and Technology na Kenya Medical Research Institute katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Nairobi, hatua inayolenga kuimarisha elimu ya juu, utafiti wa kisayansi na ubunifu nchini humo.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya mkakati wa makusudi wa kupanua fursa za elimu ya juu pamoja na kuimarisha mazingira ya utafiti na uvumbuzi yatakayosaidia maendeleo ya taifa.

Kupitia hatua hiyo, Kenya inalenga kujenga mustakabali unaotegemea elimu bora, ubunifu wa ndani na maendeleo endelevu ya tafiti mbalimbali za kisayansi.

Viongozi waliozungumza wakati wa hafla hiyo walisisitiza kuwa vyuo vikuu vina nafasi muhimu katika kuandaa wataalamu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasayansi, wahandisi, madaktari na wabunifu ambao watasaidia kuleta mabadiliko ya maendeleo nchini.

Aidha, ilielezwa kuwa pamoja na kuchangia maendeleo ya kitaifa, wataalamu hao pia wanatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika nyanja mbalimbali duniani kupitia maarifa, teknolojia na suluhisho za changamoto zinazokabili jamii.

Hatua hiyo pia inatazamwa kama juhudi za Kenya za kuimarisha sekta ya elimu na kuifanya nchi hiyo kuwa kitovu cha utafiti, teknolojia na ubunifu katika ukanda wa Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...