Katika hatua muhimu kwa sekta ya benki nchini  na uongozi wa taasisi za kibiashara barani Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ruth Zaipuna, anatarajiwa kuzungumza katika Cambridge Africa Business Conference 2026, utakaofanyika Mei 30, 2026 katika Chou cha Biashara cha Cambridge Judge chini ya  Chuo Kikuu cha Cambridge Uingereza.

Katika jukwaa hilo, Zaipuna anatarajiwa kutoa hotuba kuu kuhusu safari ya mageuzi ya NMB na mchango wake katika uchumi wa Tanzania, akieleza namna benki hiyo ilivyokua kutoka katika mizizi ya huduma ndogo za fedha hadi kuwa moja ya taasisi zinazoongoza katika sekta ya fedha nchini.

Mkutano huo wenye kaulimbiu ya “Kujenga Mustakabali wa Afrika: Mitaji, Ubunifu na Ukuaji wa Kiwango cha Bara,” unalenga kujadili nafasi ya Afrika katika kuchochea ukuaji kupitia mitaji, ubunifu na uwezo wa taasisi za Afrika kufanya kazi kwa kiwango cha bara, hususan katika mazingira ya AfCFTA.

Akizungumzia mwaliko huo, Zaipuna alisema ni heshima kwa NMB na Tanzania, akibainisha kuwa safari ya benki hiyo inaonesha kuwa taasisi zinazoongozwa na Waafrika zinaweza kujenga ubora wa kiwango cha dunia huku zikibaki karibu na mahitaji ya wananchi, biashara na vipaumbele vya taifa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...