Na Janeth Raphael MichuziTv Bungeni - Dodoma
Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha uhakiki wa madeni ya waliokuwa wafanyakazi wa Mgodi wa Kiwira kabla ya kuanza mchakato wa malipo ya madai yao yaliyodumu kwa miaka kadhaa.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa wakati akijibu swali la Mbunge wa Kyela, Baraka Ulimboka Mwamengo, ambaye alihoji ni lini Serikali itawalipa waliokuwa watumishi wa mgodi huo.
Akijibu swali hilo, Dkt Kiruswa amesema deni la wafanyakazi wa Kiwira lilitokana na malalamiko ya mapunjo ya mafao kwa wafanyakazi waliokuwa wakihudumu katika mgodi huo kabla ya kubinafsishwa.
Ameeleza kuwa baada ya malalamiko hayo kuwasilishwa na Chama cha Wafanyakazi Migodini na Ujenzi (TAMICO), Serikali kupitia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilifanya ukaguzi maalum mwezi Novemba mwaka 2008 ili kuchunguza madai hayo.
Aidha, amesema kuwa baadaye iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini iliunda timu maalum iliyofanya uhakiki mwingine wa madeni hayo mwezi Desemba mwaka 2015 kwa lengo la kubaini kiwango halisi cha madai ya wafanyakazi hao.
Dkt Kiruswa amesema matokeo ya uhakiki yalionesha kuwa madai halali ya wafanyakazi yalifikia shilingi bilioni 1.024 kwa wafanyakazi 893, tofauti na madai ya awali ya shilingi bilioni 47 yaliyokuwa yakidaiwa na watumishi 1,687.
Mbali na madai ya wafanyakazi, Serikali pia ilibaini uwepo wa madeni ya wazabuni mbalimbali, ikiwemo kampuni iliyokuwa ikitoa huduma za ulinzi katika mgodi huo, yenye madai ya takribani shilingi milioni 496.
Amesema jumla ya madeni yote yaliyohakikiwa ilifikia shilingi bilioni 1.52, ambazo ziliingizwa rasmi katika orodha ya madeni ya Serikali kwa ajili ya kushughulikiwa.
Amebainisha kuwa Wizara ya Madini inaendelea kushirikiana na Wizara ya Fedha kuhakikisha malipo hayo yanafanyika mara baada ya kukamilika kwa hatua zote muhimu za uhakiki.
Aidha, amefafanua kuwa mwaka 2025 Wizara ya Fedha ilituma timu ya wataalamu kufanya uhakiki mwingine wa mwisho ili kujiridhisha na taarifa iliyotolewa katika uhakiki wa mwaka 2015 kabla ya Serikali kuanza kulipa madai hayo.
“Kwa sasa timu ya wataalamu inakamilisha taarifa ya mwisho ya uhakiki ili kuwezesha Serikali kuanza mchakato wa kulipa madeni hayo,” alisema Waziri huyo.
Hatua hiyo imeendelea kuibua matumaini kwa mamia ya waliokuwa wafanyakazi wa Mgodi wa Kiwira ambao wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu kupatiwa haki zao baada ya madai yao kuchelewa kushughulikiwa kwa miaka mingi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...