MAMIA ya wananchi wamejitokeza  kuchangia damu  katika  kambi maalumu  iliyoandaliwa na Mbunge wa  Jimbo la Ukonga,  Bakari Shingo, viwanja vya Pugu Kajiungeni, wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, leo.

Kambi hiyo  ilianza kwa matembezi ya hisani  ya kilometa tano yaliyoanzia Mombasa  hadi viwanja vya Pugu yakiongozwa na mbunge huyo  na kushiriki, wananchi, vikundi vya jogging na makundi mbalimbali.

Akizungumza katika kambi hiyo, Mbunge Shingo, amesema dhamira ni kuchangisha damu ili kuokoa maisha ya  watu hususan wanawake wanao jifungua, waliopata ajali, wagonjwa wa kawaida na wananchi wote  wenye matatizo ya kuhitaji damu hospitalini.

 Shingo amesema  kuchangia damu ni ibada  hivyo kuwataka wananchi kuendeleza utamaduni huo bila kujali itikadi zao za kidini na kisiasa.

“Damu hii tunayo change itakwenda kuokoa wananchi wote bila kujali dini zao wala itikadi za kisiasa.  Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ukonga tunawashukuru wananchi waliojitokeza  leo kujitoleaa damu,”amesema Shingo.

 Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ambaye ni Katibu Tarafa ya Ilala, Kheri William, amempongeza Mbunge Shingo kwa kuandaa kambi hiyo na kuomba utaratibu  huo uendelezwe.

“Tunaomba mbunge  huu utaratibu ulioanzisha wa kuandaa matembezi na uchangiaji damu  uendelee. Angalau kila baada ya miezi sita tuandae kambi hii,”alisema Katibu  tarafa huyo.
Alisema katika matibabu damu haina mbadala kwani haitengenezwi  kwa namna yoyote  ispo kuwa kwa wananchi kujitolea damu yao na kuokoa maisha ya wahitaji.

Zoezi la utoaji damu lilisimamia na  maofisa  wa Mpango wa Taifa wa Damu Salamaa, kutoka Hospitali ya Rufani ya Amana, ambao wamempongeza Mbunge Shingo na wananchi wote walio fika kujitolea damu kwa kuzingatia umuhimu wa uchangiaji huo









 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...