
Meneja wa Bidhaa wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. George Kaindoah, akimkabidhi tuzo Malachi Mwiki, mmoja wa washindi wa mashindano ya kuogelea ya Swahili Talent Swimming, yaliyodhaminiwa na Benki ya Absa na kumalizika jana katika viwanja vya Gymkhana Club jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalishirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka shule zaidi ya 25, huku yakitoa kipaumbele maalum katika kuhamasisha ushirikishwaji kwa kuwajumuisha watoto wenye mahitaji maalum kutoka Dar es Salaam na Arusha, kwa lengo la kutambua na kukuza vipaji vya vijana katika mchezo wa kuogelea.

Muogeleaji chipukizi Cairo Erick Johannes, akionesha umahiri wake wakati wa mashindano ya kuogelea ya Swahili Talent Swimming, yaliyodhaminiwa na Benki ya Absa Tanzania na kumalizika jana katika viwanja vya Gymkhana Club jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalishirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka shule zaidi ya 25, huku yakilenga kuhamasisha ushirikishwaji kwa kuwajumuisha watoto wenye mahitaji maalum kutoka Dar es Salaam na Arusha, kwa lengo la kutambua na kukuza vipaji vya vijana katika mchezo wa kuogelea.

Meneja wa Bidhaa wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. George Kaindoah, akimkabidhi tuzo Amran Suleiman, mmoja wa washindi wa mashindano ya kuogelea ya Swahili Talent Swimming, yaliyodhaminiwa na Benki ya Absa na kumalizika jana katika viwanja vya Gymkhana Club jijini Dar es Salaam. Washindi wengine wanaoonekana pichani ni Alssein Humudi (wa tatu kushoto) na Konhelli Mhella. Mashindano hayo yalishirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka shule zaidi ya 25, huku yakilenga kuhamasisha ushirikishwaji kwa kuwajumuisha watoto wenye mahitaji maalum kutoka Dar es Salaam na Arusha, kwa lengo la kutambua na kukuza vipaji vya vijana katika mchezo wa kuogelea.

Waogeleaji wakichuana wakati wa mashindano ya kuogelea ya Swahili Talent Swimming yaliyodhaminiwa na Benki ya Absa Tanzania na kumalizika jana katika viwanja vya Gymkhana Club jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalishirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka shule zaidi ya 25, huku yakilenga kuhamasisha ushirikishwaji kwa kuwajumuisha watoto wenye mahitaji maalum kutoka Dar es Salaam na Arusha, kwa lengo la kutambua na kukuza vipaji vya vijana katika mchezo wa kuogelea.

Baadhi ya washiriki wenye mahitaji maalumu, wakipozi kwa picha ya kumbukumbu na Irene Mushi kutoka Benki ya Absa, baada ya kuwakabidhi medali zao, wakati wa mashindano ya kuogelea ya Swahili Talent Swimming, yaliyodhaminiwa na Benki ya Absa na kumalizika jana katika viwanja vya Gymkhana Club jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalishirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka shule zaidi ya 25, huku yakilenga kuhamasisha ushirikishwaji kwa kuwajumuisha watoto wenye mahitaji maalum kutoka Dar es Salaam na Arusha, kwa lengo la kutambua na kukuza vipaji vya vijana katika mchezo wa kuogelea.

Muogeleaji chipukizi Malikah Kassim akionesha medali yake wakati wa mashindano ya kuogelea ya Swahili Talent Swimming yaliyodhaminiwa na Benki ya Absa Tanzania na kumalizika jana katika viwanja vya Gymkhana Club, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalishirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka shule zaidi ya 25, huku yakilenga kuhamasisha ushirikishwaji kwa kuwajumuisha watoto wenye mahitaji maalum kutoka Dar es Salaam na Arusha, kwa lengo la kutambua na kukuza vipaji vya vijana katika mchezo wa kuogelea.

Baadhi ya washindi wa mashindano ya kuogelea ya Swahili Talent Swimming Competition Season 3 yaliyomalizika jana, wakionesha medali zao wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo katika viwanja vya Gymkhana Club, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalishirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka shule zaidi ya 25, huku yakilenga kuhamasisha ushirikishwaji kwa kuwajumuisha watoto wenye mahitaji maalum kutoka Dar es Salaam na Arusha, kwa lengo la kutambua na kukuza vipaji vya vijana katika mchezo wa kuogelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...