Imebainika kuwa changamoto zinazowakabili wauguzi katika Wilaya ya Bukombe zimepungua kwa kiasi kikubwa, kufuatia kupungua kwa malalamiko kutoka kwa watoa huduma na wapokea huduma katika kada ya afya.

Hayo yamebainika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, ambayo huadhimishwa kila tarehe 12 Mei. Wilaya ya Bukombe imeadhimisha siku hiyo Mei 22 mwaka huu.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Paskas Muragili, amesema kupungua kwa changamoto hizo kumetokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha huduma za afya zinaimarishwa nchini.

Mhe. Muragili amefafanua kuwa serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa wauguzi, ikiwemo kuongeza watumishi na vifaa tiba, hatua iliyosaidia kupunguza mzigo wa kazi na malalamiko.

Katika hatua nyingine, DC Muragili amesema kuwa jumla ya wauguzi 165 wameajiriwa katika mwaka wa fedha wa 2025/2026. Amemuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe kuhakikisha anawapangia vituo waajiriwa hao wapya kwa uwiano.

Amesisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha kila kituo cha kutolea huduma za afya wilayani humo kinaondokana na uhaba wa wauguzi na wananchi wanapata huduma bora kwa wakati.

Kwa upande wake, Muuguzi Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Diana Makubi, amesema malalamiko ya wauguzi na wagonjwa yamepungua kwa kiasi kikubwa. Amesema hii inatokana na uanzishwaji wa madawati maalumu yanayoshughulikia changamoto za wauguzi.

Chama cha Wauguzi Wilayani Bukombe kimekuwa kikiadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani kwa miaka minne mfululizo. Lengo ni kuwatia nguvu na kuwapa hamasa wauguzi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...