Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa Mikoa 21 ya Tanzania Bara inayotarajiwa kufanya utekelezaji wa Mradi wa Scale wenye lengo la kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea kudhihirika kila wakati na kuwa tishio kwa uzalishaji wa chakula na ustawi wa mazingira.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Bi. Aziza Mumba alipokua akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo waratibu wa Halmashauri, Mkoa na timu zinazosimamia utekelezaji wa Mradi wa Scale yanayofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jengo la Mkapa Jijini hapa Mei 04, 2026.
“Programu ya Scale ina lengo la kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yapo bayana kutokana na baadhi ya maeneo kupata mvua chini ya wastani, mfano eneo lilikuwa likipata mvua kwa siku 70 lakini limepata kwa siku 35 au chini ya hapo, pia kiasi cha mvua ni nusu ya ambacho huwa inanyesha kila mwaka, hivyo kina athiri uzalishaji ambapo tulizalisha kwa 49% chini ya lengo tulilokuwa tumepanga”.
Katika wasilisho lake juu ya utekelezaji wa Mradi huo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kati Hombolo Dr. Rogers Rugeiyamu amesema lengo kuu la Mradi ni kuimarisha Mifumo ya Serikali Kuu na Serikali za mitaa ili kuongeza ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na kuwezesha uwekezaji kwa miradi inayoibuliwa na wanajamii wenyewe katika maeneo yaliyo hatarini.
Ameongeza kuwa, Mradi huo ni wa miaka mitano kuanzia 2025/26 hadi 2030 ukihusisha Halmashauri 65 kwa Tanzania Bara na Zanzibar ambapo kwa Bara ni Halmashauri 54 na Zanzibar 11, ukitekelezwa kwa fedha za Ruzuku kwa 90% huku mchakato wa matumizi ya ukiwa shirikishi, ambapo bajeti kuu ni Dola Milioni 110 zitakazotolewa na Benki ya Dunia, 10% zitakua Ruzuku na 90% italenga matumizi ya Halmashauri.



.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...