Na.Ashura Mohamed - Arusha
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wametoa vitanda 160 pamoja na magodoro 160 vyenye thamani ya shilingi milioni 43,kwa ajili ya kusaidia waraibu wa dawa za kulevya wanaopata huduma katika nyumba za upatikanaji nafuu (Sober House),zinazoratibiwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini.
Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Dkt.Fortunatus Magambo bw. Venance Mwaijibe,amesema msaada huo ni utaratibu wa taasisi hiyo wa kusaidia jamii ambapo awamu hii imewaangukia waraibu wa Madawa ya Kulevya Jijini Arusha.
Bw.Venance amesema kuwa kazi kubwa ya mfuko wa jamii ni kukaa na jamii kwa kuwa PSSSF ni mfuko wa jamii na Waraibu wa Madawa ya kulevya ni wanajamii wenzao hivyo wana wajibu wa kuwashika mikono ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya serikali ya Kazi na Utu ili kufanya kazi kwa kujali utu,na kuhakikisha waraibu wanapambana na changamoto hiyo.
"Niseme tu PSSSF itaendelea kuwa karibu na Jamii na tutaendelea kuiunga mkono serikali yetu kwa kuendelea kuisadia jamii katatua baadhi ya changamoto sehemu nyingine tumejenga madasa,pia tumechimba visima na leo hii ni vitanda 160 na magodoro 160,ili kuwawezesha hawa wenzetu kuwa na mazingira bora ili wapone kabisa"Alisisitiza Venance
Amesema PSSSF imeamua kuunga mkono juhudi za serikali kwa kutoa vitanda na magodoro hayo ili kuboresha huduma za malazi kwa waraibu wanaopatiwa matibabu na ushauri nasaha kwani mfuko huo unaamini katika kushirikiana na jamii kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
“PSSSF tuna kauli mbiu ya ‘Leo, Kesho’. Kwa kushirikiana na NSSF tunajenga maisha ya sasa na ya baadaye, tumeungana kurejesha kwa jamii sehemu ya faida tunazopata kwa kusaidia mapambano dhidi ya dawa za kulevya ili kupata raia wema na wenye mchango chanya kwa taifa,” Alifafanua Venance
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Abubakar Mshangama, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Masha Mshomba, alisema mifuko hiyo miwili imeamua kushirikiana kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Bi.Sarah Ndaba, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa DCEA, Aretus Lyimo ameishukuru PSSSF na NSSF kwa msaada huo,akisema utasaidia kuimarisha huduma zinazotolewa kwa waraibu wanaopata nafuu kupitia nyumba hizo.
“Msaada huu utasaidia waraibu kurejea katika hali zao za kawaida na taasisi hizi zimetusaidia sana kuboresha mazingira ya waraibu wetu katika makazi yao hivyo tunaomba na wadau wengine wajitokeze kusaidia juhudi hizi kwa kuwa mazingira bora ya matibabu yanaongeza uwezekano wa mgonjwa kupona na kurejea katika maisha ya kawaida,” Alisema Sarah
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambaye ndie alikuwa awe Mgeni rasmi katika hafla hiyo CPA Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, amesema mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanawezekana kupitia ushirikiano wa wadau mbalimbali.
Amesema DCEA inaendelea kudhibiti biashara ya dawa za kulevya pamoja na kuhakikisha huduma za matibabu zinapatikana katika vituo mbalimbali hivyo kama serikali ni lazima kulinda nguvu kazi ya taifa.
Baadhi ya waraibu waliopona Baita Chacha amesema alitumia dawa za kulevya kwa miaka 15 kabla ya kupata msaada kupitia Sober House, ambapo sasa amepona baada ya kuishi katika kituo hicho kwa mwaka mmoja kwani uraibu ni changamoto ya afya ya akili inayohitaji msaada wa karibu kutoka kwa jamii na wataalamu.
Mkoa wa Arusha una jumla ya nyumba 19 zinazotoa huduma kwa waraibu ambapo katika mkoa huo kuna waraibu wapatao 505,wanawake ni 98 na wanaume ni 407.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...