Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati  ya kuboresha elimu ya michezo, pamoja na kuinua uwezo wa walimu wa fani hiyo hapa nchini, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata maarifa bora kwa maendeleo ya vipaji vyao.

Akizungumza  katika hafla ya usiku wa Tuzo kwa  Wanamichezo zilizoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  tarehe 9 Mei, 2026, Mhe.  Makonda amesema, kuna umuhimu wa kuendelea kuwajengea walimu uwezo kupitia programu maalum za mafunzo ili waendane na mahitaji ya sasa. 

Ameeleza kuwa, hatua hiyo itasaidia walimu kuelewa vizuri mbinu za ufundishaji pamoja na kuwasaidia wanafunzi kutambua vipaji vyao katika michezo  mapema.

"Serikali inalenga kuhakikisha walimu wanaopata nafasi ya kufundisha michezo  katika shule zetu wanakuwa na sifa na uelewa unaotakiwa ili kuongeza ubora wa elimu ya michezo.Tunaendelea kuboresha mazingira bora ya kazi, pamoja na motisha kwa walimu  zitakazowawezesha kufanya kazi kwa bidii" alisema Mhe. Makonda.

Ameongeza  kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na jamii pamoja na wadau mbalimbali ili kuhakikisha sekta ya michezo  inazidi kuimarika na kutoa wataalamu wenye ushindani na ubunifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...