Serikali imeendelea kuweka nguvu katika kulinda haki na ustawi wa mnyama kazi punda kutokana na umuhimu wake kwa jamii katika kusaidia shughuli za kiuchumi na kuongeza kipato kwa wananchi.

Serikali imezitaka mamlaka zote kuhakikisha zinasimamia Sheria ya Wanyama, ikiwemo kulinda punda dhidi ya ukatili na kuwachukulia hatua za kisheria wanaovunja sheria hizo, aidha imehimiza wananchi kuhakikisha wanyama hao wanapatiwa chakula, matibabu pamoja na kutobughudhiwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita katika Maadhimisho ya Siku ya Punda Duniani yaliyofanyika kitaifa katika Mtaa wa Mgusu, Manispaa ya Geita, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashimu Komba amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakipuuzia thamani ya punda huku wakimtendea ukatili mnyama huyo.

Maadhimisho hayo yameratibiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Shirika la INADES-Formation Tanzania, ASPA pamoja na mashirika mengine kwa ufadhili wa Brooke East Africa.

Komba amesema kutoweka kwa punda kutasababisha athari kubwa katika shughuli za usafirishaji pamoja na maisha ya wananchi wanaomtegemea kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Akitoa taarifa ya shughuli zilizotekelezwa kuelekea maadhimisho hayo, Daktari wa Mifugo kutoka Taasisi ya INADES, Charles Bukula amesema zaidi ya wanyama kazi 200 wamefanyiwa matibabu huku wananchi zaidi ya 1,000 wakifikishiwa elimu kuhusu utunzaji na haki za wanyama kazi.

Kwa upande wake, Kaimu Mratibu wa Huduma za Mifugo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi, Shabani Tuzzo amesisitiza umuhimu wa jamii kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha wanyama kazi wanatunzwa na kuthaminiwa.

Naye Mkurugenzi wa Brooke East Africa amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha ustawi wa wanyama kazi unaimarishwa nchini.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Wanyama Kazi wa Kata ya Mgusu, eneo hilo lina zaidi ya wanyama kazi 800 wanaotumika katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi huku wakazi wa maeneo hayo wakieleza namna wanavyomthamini mnyama huyo katika maisha yao ya kila siku.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...