Na Mwandishi Wetu.
Waziri
wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesisitiza kwamba bajeti ya wizara hiyo
kwa mwaka wa fedha 2026/27 inapaswa kutoa mwelekeo wa Taifa katika
utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.
Mchengerwa
amesema hayo Jumapili Mei 03, 2026 wakati akizungumza kwenye ufunguzi
wa kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya kilichofanyika
ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
"Lazima
tujiandae kikamilifu kwa utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa
Wote. Hili si suala la kadi pekee bali lazima kuwe na utayari wa
miundombinu, mifumo, dawa na rasilimali watu imara" alisema Mchengerwa.
Mchengerwa
alisisitiza kwamba lazima mifumo ya TEHAMA iwe imara, upatikanaji wa
dawa na vifaa tiba uimarishwe huku akiweka mkazo kwa buzalishaji wa
ndani kupewa kipaumbele na Wizara ya Afya.
"Lazima
mifumo ya manunuzi itoe kipaumbele kwa wazalishaji wa ndani. Katibu
Mkuu nakuagiza usimamie hilo, ununuzi kupitia MSD na mifumo yetu ya
manunuzi lazima izingatie hilo lakini kwa kuzingatia ubora" ameongeza.
Mchengerwa
aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali inayoongozwa
na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kupiga hatua ikiwemo
kuongeza upatikanaji wa dawa muhimu kufikia wastani wa asilimia 73 kwa
mwezi Februari, 2026.
"Pia
tumeendelea kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kupitia uwekezaji
katika vituo vya afya, hospitali za wilaya, vifaa tiba na rasilimali
watu. Haya ni mafanikio ya pamoja chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan" alisema Mchengerwa.
Pia
alitoa wito kwa kila mtumishi, kuanzia makao makuu hadi hospitali za
rufaa, kutoka idara hadi kituo cha afya, kuhakikisha wanatoa huduma kwa
weledi na huruma kwa wananchi.
"Hatutavumilia
ucheleweshaji wa huduma usio na sababu. Hatutavumilia upendeleo
unaodhalilisha haki za mwananchi" alisisitiza Mchengerwa huku akiagiza
Katibu Mkuu kufanyia kazi malalamiko ya wagonjwa kukaa muda mrefu bila
kupata huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt Seif Shekalaghe alisema
kikao hicho kimelenga kujadili na kupitisha mwelekeo wa bajeti ya wizara
hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27 yenye lengo la kuboresha huduma za afya
kwa wananchi pamoja na ustawi wa watumishi.
Naye
Katibu wa Baraza hilo, Vivian Joseph ambaye ni Afisa Tawala Mkuu Wizara
ya Afya alisema kupitia kikao hicho kitasaidia upatikanaji wa bajeti
ambayo ni shirikishi kutekelezwa na watumishi wa wizara hiyo baada ya
kupitishwa na bunge.
Waziri
wa Afya, Mohamed Mchengerwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha
baraza kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika jijini Mwanza.
Waziri
wa Afya, Mohamed Mchengerwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha
baraza kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika jijini Mwanza.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza kwenye kikao cha
baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo kilicholenga kujadili na kupitisha
bajeti ya mwaka 2026/27.
Mganga
Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe akizungumza kwenye kikao cha
baraza la wafanyakazi Wizara ya Afya kilichoketi jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya wakifuatilia kikao cha baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya wakifuatilia kikao cha baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya wakifuatilia kikao cha baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...