Katika bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, makabila ya Wadatoga na Wahadzabe ambayo ni sehemu ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai walitia nakshi na uturi bajeti hiyo kwa kumsindikiza waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) kuingia katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.
Wadatoga ni waumini wa kuoa mke zaidi ya mmoja wanaotokana na jamii yao, wana uwezo wa kuoa hadi wake kumi na kila mke akafurahia utamu wa ndoa kutoka kwa mume wake.
Kwa Jamii hii kuwa na wake wengi si heshima tu bali unachukuliwa kama uchumi kwa kuwa utapata watoto wengi watakaokusaidia shughuli za kuchunga mifugo, kulima chakula cha familia, kufanya kazi za uhunzi, kujenga maboma ya familia na kutanua ukubwa wa jina la ukoo.
Wadatoga hawaishiwi "Power" kwasababu hawali chipsi mayai, soseji wala Baga, hawatafuti energy wala dawa za Congo,hawana mawazo ya vikoba,ni mwendo wa vyakula vya asili tu kama Ugali, mtama, ulezi, Maharage, mbaazi, viazi vitamu na Maziwa ambapo mafuta ya kupikia hawanunui dukani bali yanatokana na samli kutoka kwenye maziwa ya Ng'ombe yaliyogandishwa kisha kuchekechwa kwenye kibuyu maalum na kuzalisha mafuta ambayo husafishwa kiasili na kukaa muda mrefu bila kuharibika.
Kama wewe ni kijana na unataka kuwa na uwezo wa kuwa na wake wengi karibu makumbusho ya Urithi Jiopaki ujue siri ya wadatoga na vyakula vyao vya miaka na mikaka.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...