Na MWANDISHI WETU
TAASISI ya Saratani Ocean Road, imeungana na taasisi nyingine za afya katika banda la Wizara ya Afya katika viwanja vya Posta, Kijitonyama, kuangalia fainali ya UEFA Champion Leage.
Fainali hiyo ya UEFA inazikutanisha miamba ya soka barani Ulaya, Arsenal ya Ungereza na PSG ya nchini Ufaransa, ambapo mashabiki wengi wa Arsenali nchini Tanzania walijitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao.
Mashabiki hao wa Asernal walioudhuria katika viwanja hivyo walipata nafasi kupima afya zao katika banda la Taasisi ya Ocean Road pamoja na kupewa elimu kuhusu ugonjwa wa saratani.
Katika shangwe hizo mashabiki wengi walijitokeza kipima afya zao pamoja na kupata elimu kuhusu saratani mbalimbali kutoka Taasisi ya Saratani Ocean.
Wananchi wametakiwa kupima mara kwa mara kujua mwenendo wa afya zao, ikiwemo saratani mbalimbali, kwasababu saratani ukigundulika mapema ni rahusi kutibika.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...