MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Women Empowement Network (TAWEN) Balozi Amina Salum Ali, amesema viongozi na watumishi wanao wajibu kuhakikisha taasisi zao zinakuwa mfano wa kuigwa kutekeleza maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na sera ya kitaifa ya nishati safi.
Ameyasema hayo leo katika semina maalumu ya matumizi ya nishati safi, iliyoandaliwa na TAWEN na kushirikisha wakuu wa shule za sekondari za Wilaya ya Ubungo na wadau wa nishati na taasisi za kifedha.
Balozi Amina, amesema watumishi wanapaswa kuwa mabalozi wa mabadiliko hayo ya kuachana na nishati chafu na kuhamasisha familia na jamii zinazo wazunguka kutumia nishati safi.
Amesema dhamira ya Rais Dk. Samia, ambaye ni kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ni kuona jamii nzima ya watanzania inatumia nishati hiyo ambapo taasisi za elimu haziwezi kuachwa nyuma.
"Hivyo basi nyie wakuu wa shule ni watu muhimu katika kusaidia jitihada hizo za Rais Dk. Samia, kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutumianishati safi. Tunataka kila mtu katika jamii atumie fursa hii. Tumsaidie rais kuibeba ejenda hii muhimu,"ameeleza Balozi Amina.
Ameeleza, Rais Dk. Samia, ametoa maelekezo kwa taasisi zikiwamo shule za bweni kutumia nishati safi hivyo kupongeza TAWEN kutoa elimu hiyo kwa wakuu wa shule ambao ni wadau muhimu wa utekelezaji wa ajenda hiyo.
"Vilevile ninaipongeza TAWEN kwa kazi kubwa ya kuunganisha wadaiu, kuendesha makongamano ya kitaifa na kimataifa na kuhamasisha uwekezaji katika nishati safi. Hii ni ishara ya uongozi thabiti na dhamira ya kweli kuleta mabadiliko chanya kwa taifa letu,"ameeleza.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Tawen, Florence Masunga, amesema lengo la semina hiyo ni kuhamasisha wakuu wa shule kutumia nishati safi shuleni, kuwapa fursa zinazo patikana kupitia uwekezaji katika nishati safi na fursa za kifedha hususan uwekezaji.
"Pia semina hii ili lenga kuwapa elimu wakuu wa shule ambayo itawafanya kuwa mabalozi wazuri wa matumizi ya nishati safi na kusaidia serikali chini ya Rais Dk. Samia, kufikia malengo ya watu wote katika jamii yetu kutumia nishati hii,"amesema Masunga.
Ameeleza, sekta ya nishati safi ina firsa nyingi ambapo wakuu wa shule wanaweza kuwekeza na kujiingizia kipato kitakacho wasaidia hata baada ya kustaafu.
Ameeleza TAWEN itaendelea kutoa elimu hiyo kwa jamii nzima ya kitanzania na hata nje ya nchi kwa kuibeba ajenda hiyo muhimu iliyoasisiwa na Rais Dk. Samia, ambayo inasaidia pia kulinda mazingira, kudumisha afya na ustawi wa jamii salama.
Ofisa Elimu ya Sekondari wa Wilaya ya Ubungo, Benedict Sandy, amewahimiza wakuu wa shule kuanza kutekeleza maelekezo ya serikali ya kutumia nishati safi na kwamba semina hiyo iwe chachu kwao.
"Tunawashukuru TAWEN kwa semina hii. Sasa iwe chachu kwetu kuanza utekelezaji wa maagizo ya serikali na kuibeba ajenda ya Rais Dk. Samia. Tuwe mabalozi, tuipeleke elimu hii kwa wanafunzi nao waipeleke katika jamii,"alisema Sandy.
Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki semina hiyo ni Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Benki ya NMB, UTT Amis, Taifa Gas na PSSSF.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...