Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema msimu wa Kipupwe wa Juni hadi Agosti (JJA) mwaka 2026 unatarajiwa kutawaliwa na hali ya baridi katika maeneo mengi ya nchi, huku mwezi Julai ukitajwa kuwa na vipindi vya baridi kali zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza utabiri huo, leo Mei 25, 2026 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema maeneo mbalimbali ya Tanzania yatashuhudia viwango tofauti vya hali ya joto, upepo pamoja na vipindi vya mvua nje ya msimu.
Dkt. Chang’a amesema hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika Kanda ya Ziwa Victoria, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kusini, Nyanda za Juu Kusini-Magharibi pamoja na Mkoa wa Singida.
Aidha, maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini na maeneo ya nchi kavu, Nyanda za Juu Kaskazini-Mashariki, Ukanda wa Pwani ya Kusini pamoja na Mkoa wa Dodoma yanatarajiwa kuwa na hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani.
Mbali na hali ya baridi, Dkt. Chang’a amesema baadhi ya maeneo yatapata vipindi vya mvua nje ya msimu, hususan maeneo ya Ukanda wa Ziwa Victoria, hasa Mkoa wa Mara, maeneo ya mwambao wa pwani na maeneo ya nchi kavu, visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na maeneo yenye miinuko katika Nyanda za Juu Kaskazini-Mashariki.
"Msimu wa Kipupwe wa mwaka 2026 unatarajiwa kutawaliwa na upepo wa Kusini Mashariki uliopungua nguvu kidogo kama ilivyo kawaida katika maeneo mengi ya nchi huku vipindi vya upepo mkali kutoka kusini vinatarajiwa kujitokeza zaidi katika miezi ya Juni na Julai, hasa katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi na maeneo ya nchi kavu. Amesema.
Amesema maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria yanatarajiwa kuwa na kiwango cha joto la chini kati ya nyuzi joto 10°C hadi 19°C, wakati Ukanda wa Pwani ya Kaskazini ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na Zanzibar unatarajiwa kuwa na kiwango cha nyuzi joto 18°C hadi 25°C kwa maeneo ya mwambao na visiwani.
Katika maeneo ya Nyanda za Juu Kusini-Magharibi, ambayo yanajumuisha Mbeya, Njombe, Songwe, Iringa na Rukwa, viwango vya joto la chini vinatarajiwa kufikia kati ya nyuzi joto 6°C hadi 21°C, huku maeneo ya miinuko yakitarajiwa kushuka chini ya nyuzi joto 5°C.
Dkt. Chang’a amesema, kufutia hali hiyo uwezekano wa kujitokeza kwa magonjwa yanayohusiana na hali ya baridi, ikiwemo homa ya mapafu kwa binadamu pamoja na magonjwa ya mifugo yanaweza kujitokeza vumbi litakalosababishwa na upepo katika baadhi ya maeneo linaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya macho, mafua na matatizo mengine ya kiafya yanayohusiana na mfumo wa upumuaji.
Kwa wafugaji, mamlaka hiyo imeonya kuhusu uwezekano wa upungufu wa maji na malisho, huku ikiwataka kuendelea kufuata ratiba za kuogesha mifugo na ushauri wa wataalamu wa mifugo ma wakulima wameshauriwa kuzingatia ushauri wa maafisa ugani katika maeneo yatakayopata vipindi vya mvua nje ya msimu.
Sekta za ujenzi, uchukuzi na madini zinatarajiwa kunufaika na hali ya hewa ya msimu huo, huku watumiaji wa bahari wakitakiwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa ili kupunguza athari za upepo unaotarajiwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...