Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma imewataka watu wenye changamoto ya kusikia kutumia elimu ya kodi kama nyenzo ya kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya Taifa, huku ikisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki katika kujenga Taifa kupitia ulipaji wa kodi kwa hiari kulingana na sheria na taratibu zilizowekwa.

Akifungua semina ya elimu ya kodi kwa jamii ya watu wenye changamoto ya kusikia  Mei 11, 2026 jijini Dodoma, Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Bw. Pendolake Elinisafi, amesema Serikali inaendelea kuhakikisha huduma za kodi zinawafikia wananchi wote kwa usawa ili kuongeza uelewa wa masuala ya kodi na kuwajengea uwezo wa kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Amesema kodi ni nguzo muhimu ya maendeleo ya Taifa kwani fedha zinazokusanywa kupitia kodi husaidia kugharamia huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, barabara pamoja na huduma nyingine muhimu zinazogusa maisha ya wananchi kila siku.

Aidha, amepongeza ushiriki wa watu wenye changamoto ya kusikia katika semina hiyo huku akiwahimiza kutumia fursa hiyo kuuliza maswali, kutoa maoni na kujifunza zaidi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa semina hiyo wameishukuru TRA kwa kuandaa mafunzo hayo wakisema yatawasaidia kuelewa vyema masuala ya kodi na namna ya kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo bila vikwazo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...