Mkoa wa Geita umeanzisha mradi mkubwa wa ujenzi wa ghala la madawa katika Halmashauri ya Chato, ambalo linatarajiwa kuhudumia mikoa ya Kagera, Shinyanga na Kigoma mara litakapokamilika. 

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani Chato, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela, alisema jengo hilo linagharimu zaidi ya shilingi bilioni 19. Ghala hilo lina ukubwa wa mita za mraba 5,000 na litahifadhi madawa pamoja na vifaa tiba kwa ajili ya vituo vya afya katika mikoa mitatu ya jirani.

Mradi huo unatekelezwa na Taasisi ya Serikali ya Medical Stores Department, MSD, na unahusisha ujenzi wa ghala pamoja na ofisi za utawala. Kwa mujibu wa mkandarasi wa mradi, Patric Laibo, ujenzi ulianza Agosti 20, 2025 na umefikia asilimia 57. Anatarajia kukamilisha kazi hiyo ifikapo Oktoba 19 mwaka huu.

Viongozi mbalimbali wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwaletea huduma hiyo wananchi wa Chato na mikoa jirani. Wamesema awali wananchi walilazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta madawa kila yanapokuwa yameisha.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...