Kampuni ya mawasiliano ya Yas imefungua rasmi duka jipya la huduma katika eneo la Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kifedha kwa wakazi wa Zanzibar.
Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni eneo la Nungwi - Zanzibar na kuongozwa na Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa ya Wilaya ya Kaskazini A’ Unguja, Mhe. Nyange Kher Ali, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Nyange Kher Ali aliipongeza Yas kwa kuendelea kuwekeza Zanzibar na kusaidia jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za mawasiliano pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.
“Uwekezaji huu una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wananchi wetu pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu za kidijitali,” alisema Mhe. Nyange Kher Ali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Uendeshaji wa Yas, Bi. Mwangaza Matotola, alisema kufunguliwa kwa duka hilo ni sehemu ya mkakati wa kampuni wa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na kuendelea kuimarisha uchumi wa kidijitali nchini.
“Uzinduzi wa duka hili hapa Nungwi ni sehemu ya mkakati wetu wa kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za mawasiliano na kifedha kwa urahisi, haraka na kwa viwango vya hali ya juu,” alisema Bi. Matotola.
Alisema Yas imeendelea kuwekeza katika upanuzi wa miundombinu yake nchini kupitia teknolojia za 4G na 5G, huku kampuni hiyo ikiwa na zaidi ya minara 4,800 inayohudumia zaidi ya wateja milioni 31 Tanzania Bara na Zanzibar.
Bi. Matotola alisema Nungwi ni eneo muhimu kiuchumi kutokana na shughuli za utalii, uvuvi na biashara, hivyo uwepo wa duka hilo utasaidia wananchi na wafanyabiashara kupata huduma kwa ukaribu zaidi.
Aidha, aliwahamasisha wananchi kutumia applikesheni mpya ya Yas inayowezesha upatikanaji rahisi wa huduma mbalimbali kidijitali.
Duka la Nungwi linaungana na mtandao wa zaidi ya maduka 556 ya Yas yaliyopo nchini kote, yakilenga kuboresha huduma kwa wateja na kuongeza upatikanaji wa huduma za kidijitali kwa Watanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...