Na Anne Robi, Mtwara.

WANAFUNZI wa Majukwaa ya sekta ya mafuta na Gas (Oil and Gas Clubs) Mkoani Mtwara wameliomba Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini  (TPDC) kuwaandalia ziara ya kutembelea miradi ya gesi asili kujifunza  kwa kuona namna gesi asilia inavyotumika kwenye magari na viwandani.

Wanafunzi hao wametoa wito huo leo tarehe 18 Mei, 2026 wakati wa mkutano wao na  shirika la TPDC waliotembelea majukwaa hayo kukagua maendeleo.

Mwanafunzi  kutoka shule ya sekondari Magamba Loveness Japhet amesema kupitia majukwaa shuleni wanapata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya gesi asilia huku akiomba wanafunzi kuwezeshwa kufika kwenye miradi ya utekelezaji wa shughuli za TPDC kujifunza zaidi.

Mwalimu Mlezi wa Jukwaa la wanafunzi sekta ya mafuta na Gesi, shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoani Mtwara, Aurelia Kimaro amesema wanafunzi wengi wanashauku ya kutaka kujua namna ambavyo gesi asilia inatumika kwenye magari na viwandani kuzalisha bidhaa mbalimbali.

"Wengi tunavyojua masuala ya gesi asilia ni mapana sana, kuna uchimbaji, utachakataji na pia utumiaji, tunaliomba Shirika la TPDC kuwaandalia wanafunzi ziara kwenye miradi ya utumiaji gesi hiyo kama viwandani na kwenye magari ili wanafunzi wajionee na kujifunza," amesema.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi  TPDC, Ali Muluge  amesema wanawawezesha wanafunzi ambao wanajiunga na majukwaa ya Mafuta na Gesi kupata elimu kwa kuwapa mahitaji ya kujifunzia na kuwawezesha kufika kwenye miradi mbalimbali ya uchimbaji, na utachakataji.

"Tumepokea ombi la wanafunzi hao kutaka sasa kufika kwenye miradi ambayo inajihusisha na utumiaji wa gesi kama vile viwandani, na tutalifanyia kazi, " amesema.

Amesema TPDC ilianzisha majukwaa ya mafuta na Gesi kwenye shule za sekondari 16 Mikoani Mtwara kwa lengo la kutoa taarifa na elimu sahihi kwa wanafunzi na walimu kuhusu shughuli za serikali kwenye sekta ya mafuta na Gesi.

"Lango lingine la kuanzisha majukwaa haya (Oil and Gas Clubs) ni kuchochea ari ya wanafunzi kupenda kusoma masomo ya Sayansi na kupata wataalamu ambao watalisaidia taifa kutekeleza shughuli kwenye sekta ya mafuta gesi," amesema.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...