WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unaofanyika leo Jumanne Mei 26, 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kintele (Kintele Congress Centre) jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.
Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na taasisi hiyo.
Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo unaowakutanisha viongozi mbalimbali wa Afrika pamoja na wadau wa maendeleo kujadili masuala ya uchumi, uwekezaji na maendeleo ya bara la Afrika.





.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...