Na Victor Masangu, Kibaha
Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini katika kusherekea miaka 48 ya maadhimisho ya wiki yao ya wazazi ngazi ya Wilaya imeamua kufanya shughulio mbali mbali za kijamii katika shule ya sekondari Bundikani ikiwemo kufanya zoezi laa upandaji wa miti ikiwa pamoja na kutoa zawadi na tuzo mbali mbali kwa walimu pamoja na wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo yao.
Katika sherehe za maadhinmisho hayo ambazo zilikwenda sambamba na matukio mbali mbali ya ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu zilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Chama pamoja na jumuiya zake ikiwemo viongozi wa serikali wakimwemo wanafunzi, walimu pamoja na wazazi na walezi.
Katibu wa Jumuiya hiyo ya wazazi Latifa Semweza amesema kwamba wameamua kutumia wiki hiyo kwa kwenda kutembelea shule ya sekondari Bundikani kwa lengo la kuweza kuwapa motisha zaidi walimu pamoja na wanafunzi kwani wamekuwa wakifanya vizuri sana katika sekta ya elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.
"Tupo katika sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa kwa jumuiya yetu ya wazazi na tumetimiza miaka 48 tangu ilipozaliwa na leo hii tymeongozana na viongozi wenzangu mbali mbali n atumekuja katika shule ya Sekondari Bundikani na tumeweza kuendesha zoezi laa kupanda miti mbali mbali ikiwemo ya maatunda pamojaa na miti ya kivuli ikiwa sambamba na kutoa motisha ya zawadi kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika masoma," amebainisha Katibu Latifa.
Kadhalika Katibu huyo amebainisha kuwa katika wiki yao ya wazazi kata zote 14 zilizopo katika Wilaya ya Kibaha mjini tayari zimeshafanya maadhimisho yao na kwamba katika ngazi ya Wilaya wao wameamua kufanya sherehe hizo katika shule ya sekondari Bundikani na lengo kubwa ni kuweza kuboresha sektya ya elimu pamoja na suala zima la upandaji wa miti ambayo itasaidia kuboresha utunzaji wa mazingira.
Katika hatua nhyingine Katibu huyo amesema kwamba katika jumuiya yao wamepewa malengo mbali mbali kwa ajili ya kuyatekeleza ikiwemo suala la kusimamia elimu kuanzia ngazi ya msingi, sekondari,pamoja na vyuo,ikiwa pamoja na kusimamia sekta ya afya, elimu pamoja na malezi.
Naye Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Kibaha mjini Yahaya Mtonda amesema kwamba waatendelea kushirikiana bega kwa bega na walimu na wanafunzi wa shule mbali mbali za msingi na sekondari lengo kubwa ikiwa ni kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaeneleo katika kuongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka aliwahimiza wanafunzi wa shule hiyo ya bundikani kuweka misingi imara katika kuingeza juhudi ya kufanya vizuri katika masomo yao ikiwemo kusoma kwa bidii kwa lengo la kufanya vizurii katika mitihani yao.
Nao baadhi ya wanafunzi wanaosoma kaatika shule hiyo ya sekondari Bundikani pamoja naa walimu wao hawakusita kutoa shukrani zao za kipekee kwa Jumuiya hiyo ya wazazi kwa kuona umuhimu mkubwa wa kwenda kutimia wiki ya sherehe za maadhimisho yao kwa kuwatembelea na kuwapa motisha ya zawadi mbali mbali hali amabyo wamesema imewapa molali zaidi katika kufanya vizuri katika elimu.
Jumuiya ya wazazi inasherekea maadhimisho ya miaka 48 tangu ilipozaliwa rasmi na kauli mbiu ya mwaka huu wa 2026 ikiwa inasema kwamba malezi bora na uzalendo ni msingi wa Taifa.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...