Na Janeth Raphael MichuziTv Bungeni - Dodoma

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Paschal Katambi Patrobass ameliomba Bunge kuidhinisha jumla ya Shilingi trilioni 2.44 kwa ajili ya matumizi ya Wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo Kwa mwaka  2036/2027 bungeni leo, Waziri Katambi amesema wizara inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,443,215,927,000 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kiusalama, kiutawala na maendeleo nchini.

Katambi ameeleza kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi 1,953,366,486,000 sawa na asilimia 80 ya bajeti yote ya wizara zitatumika kwa Matumizi ya Kawaida.

Amefafanua kuwa ndani ya fedha hizo, Shilingi 1,183,766,640,000 zimetengwa kwa ajili ya mishahara ya watumishi, huku Shilingi 769,599,846,000 zikielekezwa kwenye matumizi mengineyo ya wizara na taasisi zake.

Aidha, Waziri huyo amesema Shilingi 489,849,441,000 sawa na asilimia 20 ya bajeti yote zimetengwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Kwa mujibu wa Katambi, kati ya fedha za maendeleo, Shilingi 453,955,843,000 ni fedha za ndani huku Shilingi 35,893,598,000 zikiwa ni fedha za nje zitakazosaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri Katambi amesisitiza kuwa fedha hizo zitawezesha wizara kuendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao, kuboresha miundombinu ya vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.

Hotuba hiyo imewasilishwa bungeni leo wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...