Kijana Joseph Mtei mwenye mahitaji maalum ambaye kwa sasa anafanya kazi katika kampuni tangu ya UJUZI katika kiwanda cha kutengeneza samani cha VETA Dodoma, amepongeza uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kumuwezesha kupata ajira rasmi.
Agizo hilo lilitolewa Juni 23, 2026, wakati wa kilele cha wiki ya utumishi wa umma Jijini Dodoma na Waziri wa TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe, ambaye alimwelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora, kuhakikisha Joseph Mtei anapatiwa ajira rasmi, amesema hatua hiyo imeonyesha kuwa serikali inatambua uwezo wa watu wenye ulemavu na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Michuzi TV Juni 24, 2026, jijini Dodoma, Mtei alisema safari yake ya maisha imekuwa ya changamoto nyingi tangu utotoni na licha ya kuzaliwa bila mikono lakini hakukata tamaa, Ameeleza kuwa elimu na mafunzo ya ufundi vimemwezesha kujijengea uwezo wa kufanya kazi na kujitegemea kama ilivyo kwa watu wengine wasiokuwa na ulemavu.
Joseph amesema fursa hiyo inapaswa kuwa chachu kwa vijana wengine wenye mahitaji maalum kuendelea kupambana na changamoto zinazowakabili na kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo, ameeleza kuwa mafanikio yake ni matokeo ya juhudi binafsi, msaada alioupata kwa baadhi ya wadau waliomsapoti kupata elimu pamoja na mazingira yaliyomruhusu kuonyesha uwezo wake kazini.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi na jamii kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu na badala yake kuwapa nafasi ya kusoma, kujifunza na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi, amesema kwa sasa anaishi maisha ya kujitegemea, analipa kodi, anamsomesha mdogo wake, jambo linalothibitisha kuwa ulemavu si kikwazo cha mafanikio.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...