NALA - DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetekeleza ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 1.6 kutoka barabara kuu ya Bahi hadi Hospitali ya Jiji, hatua inayolenga kuboresha huduma za afya na kiuchumi kwa wananchi wa Kata ya Nala.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2026, Wazo Mwang’onda alipongeza mradi huo na kusema kuwa ni bora, umekidhi vigezo vyote muhimu kama taratibu za ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami zinavyotaka.
Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru umeridhishwa na ujenzi huo na upo tayari kuizindua. “Mwenge wa Uhuru umeridhishwa na ujenzi huu wa barabara ya Kilomita 1.6 ambayo imekamilika kwa ubora wa hali ya juu na sasa upo kwenye matazamio ya mwisho, umeridhishwa na namna barabara hii imejengwa. Tunaamini wakazi wa eneo hili watanufaika sana na uwepo wa barabara hii" alisema Mwang’onda.
Awali akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara hiyo, Mhandisi wa Miradi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mha. Nicodemus Kileo alisema kuwa mradi huo ulitekelezwa na mkandarasi mzawa M/s. Kings Builders Limited kwa gharama ya shilingi bilioni 2.87 zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, na upo tayari kuzinduliwa.
Nae, Mkazi wa Nala, Gervazi Sebastian alipongeza ujenzi wa barabara hiyo akieleza kuwa imeondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa Nala. "Tunaishukuru sana serikali kwa kutujengea hii barabara, awali ilikuwa ngumu kupata usafiri wa nafuu kwasababu barabara ilikua mbovu. Kwakweli serikali imetuokoa hata huduma zingine zinapatikana kwa urahisi" alisema Sebastian.
Katika hatua nyingine, Mkazi wa Mtaa wa Segu Chini, Asia Omari alipongeza ujenzi wa barabara hiyo akisema kuwa imekuwa mkombozi kwa watumiaji hasa wanawake wajawazito wanaopita kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Jiji la Dodoma.
Mradi huo ni miongoni mwa miradi iliyozinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi na Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2026 uliobeba kaulimbiu isemayo “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo”.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...