KATIKA kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, wafanyakazi wa Benki ya Absa kwa kushirikina Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), wamepanda miti 1300  katika Msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Wilayani Kisarawe, mkoani Pwani mwishoni mwa wiki huku benki hiyo ikiahidi kuyafanya matukio hayo kuwa endelevu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga alisema suala la upandaji miti ni jambo muhimu sana katika suala zima la uhifadhi wa mazingira kutokana na faida mbalimbali zinazotokana na misitu.    

“Benki ya Absa lengo lake kuu linasema ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, Hatua Moja Baada ya Nyingine’, kwa kupanda miti katika eneo hili la Pugu Kazimzumbwi, tunaamini tunasaidia kuwawezesha wakazi wa Dar es Salaam kuwa na afya njema inayotokana na hewa safi kutoka mahali hapa kwani Kazimzumbwi ndio mapafu yanayolifanya jiji la Dar es salaam lipumue kwa kufyonza hewa chafu inayotoka humo.

“Absa pia tunasema, Stori yako ina Thamani’ tunaamini kila stori ya mtanzania ina thamani sana kwetu, hivyo kwa kuja kupanda miti tukishirikiana na Shirika la WWF, tunaamini tumekuja kuandika Stori ya Jiji la Dar es salaam kwa kuhakikisha kwamba miti hii tunayopanda inawezesha utoaji wa hewa safi, kuleta chanzo cha mvua na kuleta mandhari nzuri na kuwa sehemu nzuri ya kutembelea,” alisema Bw. Luhanga.

 Naye Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), Bw. Manyerere Wajama, akimwakilisha mkurugenzi wa shirika hilo katika hafla hiyo alisema kwa kushirikia na Benki ya Absa tukio ni uwekezaji mkubwa katika suala la hewa safi na utunzaji wa mazingira, na pia msitu huo ni rasilimali kubwa kwa wakazi wa Kisarawe,  kwenye hewa safi kwa sababu msitu unanyonya hewa chafu, kwenye ecology ya mazingira na pia msitu wa Pugu Kazimzumbwi  ni muhimu kwenye kusaidia shughuli za wananchi wa eneo la kisarawe na maeneo Jirani.

“Kwa kupanda miti tunawekeza katika maisha ya baadae ya watoto wetu, kwa sababu kwa kuhifadhi mazinigira leo tunategemea watu wataendelea kuishi kwenye mazingira safi na salama, tunahitaji ushirikiano, serikali, sekta binafsi pamoja na wakazi wa eneo hili, leo tukiondoka mwanajamii akaingiza mifugo yake maeneo haya tunakuwa hatujafanya kitu chochote,  kwahiyo ili kazi yetu iwe na maana tunatakiwa tushirikiane,” alisema Bw. Wajama akitoa shukurani kubwa kwa Benki ya Absa kwa kuwa wadau wao muhimu katika suala la uhifadhi wa mazingira.

Awali Naibu Ofisa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Bw. Idd Mbaruku alisema zoezi la upandaji wa miti 1300 kutoka Benki ya Absa wakishikiana na WWF ni muendelezo wa jitihada ya utunzaji wa mazingira hasa katika hifadhi yao ya Pugu Kazimzumbwi huku wakishirikiana karibu na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

“Kama inavyoelezwa msitu huu ndio mapafu ya jiji letu la Dar es Saalam, lakini pia ndio mbavu za wilaya yetu ya Kisarawe kutokana na umuhimu wake kwa sababu hapa tupo karibu sana na Dar es salaam na kama tunavyojua jiji hilo lina viwanda vingi, kuna mchafuko mkubwa wa hali ya hewa, kwahiyo msitu huu umekuwa ni sehemu ya kufyonza hiyo hewa chafu, kwa hiyo sisi kama serikali kwa kushirikiana na jamii inayotuzunguuka tutahakikisha miti hii iliyopandwa inazidi kukua,” alisema Bw. Mbaruku.

Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga (kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidigitali wa Benki ya Absa Tanzania, Samuel Mkuyu ( katikati ), na Mhifadhi Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Bw. Baraka Mtewa wakishirikiana kupanda miti kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani, kwa kushirikiana na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), katika msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Wilayani Kisarawe, mkoani Pwani jana. Benki ya Absa imepanda miti 1300 ikishirikiana na shirika hilo.

Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga (kushoto), na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidigitali wa Benki ya Absa Tanzania, Samuel Mkuyu, wakipanda miti kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani, kwa kushirikiana na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), katika msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Wilayani Kisarawe, mkoani Pwani jana. Benki ya Absa imepanda miti 1300 ikishirikiana na Shirika la WWF.

Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), Bw. Manyerere Wajama, wakipanda miti kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani, katika msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Wilayani Kisarawe, mkoani Pwani jana. Benki ya Absa imepanda miti 1300 ikishirikiana na Shirika la WWF.

Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kulia), Mhifadhi Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Bw. Baraka Mtewa na Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), Bw. Manyerere Wajama, wakishirikiana kupanda miti kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani, katika msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Wilayani Kisarawe, mkoani Pwani jana. Benki ya Absa imepanda miti 1300 ikishirikiana na Shirika la WWF.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania walipanda miti, kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani, kwa kushirikiana na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), katika msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Wilayani Kisarawe, mkoani Pwani jana. Benki ya Absa imepanda miti 1300 ikishirikiana na shirika hilo.
Wafanyakazi na viongozi wa Benki ya Absa Tanzania, wawakilishi kutoka Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), Viongozi wa Kiserikali kutoka Wilaya ya Kisarawe, wawakilishi kutoka Ofisi ya Misitu wilaya, Wakala wa Misitu (TFS), na wadau wengine wa mazingira wakipozi kwa picha ya kumbukumbu muda mfupi baada ya kukamilika kwa zoezi la upandaji miti katika Msitu wa Pugu Kazimzumbwi, Wilayani Kisarawe, Mkoani Pwani jana, kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...