Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, ameendelea na ziara yake ya kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii mkoani Mtwara.
Akiwa katika shughuli za ubanguaji korosho, Ndugu Rabia amesema CCM itaendelea kusimamia na kulinda maslahi ya wakulima wa korosho, akibainisha kuwa zao hilo lina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wananchi na Taifa.
Aidha, ameelekeza kuchimbwa kwa kisima cha maji katika eneo la Mtwanya Juu ili kusaidia shughuli za Kiwanda cha Ubanguaji Korosho.
“Serikali ya CCM haitorudi nyuma katika kulinda maslahi ya mkulima wa korosho. Mkulima anapostawi, Taifa linastawi. Tuendelee kuzalisha kwa wingi na kwa ubora zaidi ili kuongeza tija na manufaa kwa wakulima,” amesema Rabia.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...