Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigela, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kubuni na kutekeleza miradi mipya ya kuongeza mapato, badala ya kuendelea kutegemea mapato ya madini peke yake.

Ametoa maelekezo hayo wakati wa Kikao Maalum cha Baraza cha kusikiliza na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali [CAG]kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2026.

Halmashauri ya Bukombe imepongezwa kwa kufaulu kupata Hati Safi katika ukaguzi wa CAG. Hati hiyo ni alama ya juu zaidi inayothibitisha kuwa fedha za umma zimetumika kwa uwazi na kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG, jumla ya hoja 24 zilibuliwa kwa mwaka 2026. Kati yake, hoja 5 zimeshatekelezwa na hoja 19 zinaendelea kutekelezwa

Mkuu wa Mkoa amewataka Madiwani kuacha tabia ya "kutengeneza hoja" ili zijibiwe, na badala yake kuzuia mapungufu kabla hayajatokea ili kuitunza taswira ya Serikali.

Halmashauri hiyo imefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 5 za mapato ya ndani, sawa na asilimia 136.3 ya lengo. Hatua hiyo imeipatia sifa Halmashauri hiyo kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Mohammed Gombat.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, Mhe. Erick Kagoma, kwa niaba ya Madiwani, amesema amepokea na atatekeleza maelekezo ya kupunguza idadi ya hoja zinazoibuliwa na CAG katika miaka ijayo.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...