MBUNGE wa Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akichangia hotuba ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum leo Juni 1,2026 bungeni jijini Dodoma.



MBUNGE wa Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akichangia hotuba ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum leo Juni 1,2026 bungeni jijini Dodoma.

......

MBUNGE wa Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, ameitaka Serikali kuboresha mazingira ya kazi kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini ikiwemo kuwapatia magari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Akichangia hotuba ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum bungeni, Dkt. Jafo amesema maafisa hao ni nguzo muhimu katika kusukuma maendeleo ya jamii na wanastahili kuwezeshwa kwa vitendea kazi vinavyokidhi mahitaji ya kazi zao.

Amesema Maafisa Maendeleo ya Jamii ni mawakala wa mabadiliko katika jamii kwa kuwa karibu kila programu ya maendeleo inayotekelezwa nchini inahitaji ushiriki wao wa moja kwa moja, hivyo ni muhimu kupewa heshima na mazingira bora ya kufanyia kazi.

Dkt. Jafo ameeleza kuwa pamoja na magari, maafisa hao wanapaswa kuwa na ofisi zenye hadhi na rasilimali za kutosha zitakazowawezesha kuwafikia wananchi kwa urahisi na kutoa huduma stahiki.

Aidha, ameishauri Serikali kuanzisha vitengo vya Maendeleo ya Jamii katika wizara zote na taasisi za umma zaidi ya 325 ili kuhakikisha masuala ya maendeleo ya jamii yanapewa kipaumbele na kuratibiwa kwa ufanisi katika sekta mbalimbali.

Pia amependekeza kuanzishwa kwa Kitengo cha Uratibu wa Sekta ndani ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii kitakachosaidia kuunganisha taarifa za maendeleo kutoka wizara na taasisi mbalimbali, hatua ambayo alisema itaiwezesha nchi kuwa na mfumo imara wa kufuatilia maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...