Equity Group imeongoza na kuandaa ziara ya Biashara na Uwekezaji wa siku nne nchini Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia tarehe 29 Juni hadi 2 Julai 2026, ukiwaleta pamoja wawekezaji, wafanyabiashara na viongozi wa biashara kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na kwingineko. 

Msafara huo umebuniwa kuonesha fursa za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania, ikiwa ni moja ya chumi zinazokua kwa kasi zaidi Afrika Mashariki, huku ukilenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kufungua milango mipya ya uwekezaji.

Kama sehemu ya ziara hiyo, Equity Group iliandaa Kongamano la Biashara katika Ukumbi wa Mfalme, kwenye viwanja vya Maonesho ya Sabasaba, kwa ushirikiano na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). 

Kongamano hilo liliwakutanisha wawekezaji wa kimataifa na biashara za ndani, pamoja na kuwezesha majadiliano kati ya sekta binafsi na Serikali kuhusu fursa za biashara, uwekezaji na ukuaji wa viwanda. 

Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Sempeho Manongi, alisisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi, biashara na uwekezaji, sambamba na ajenda ya taifa ya ukuaji wa viwanda na biashara ya kikanda.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mkuu wa Wateja Wadogo, wa Kati na Binafsi wa Equity Bank Tanzania, Bi. Theresia Mayanie, alisema Equity inaendelea kuwa daraja muhimu kati ya mitaji na fursa kwa kuwaunganisha wawekezaji na biashara za ndani kupitia huduma za ushauri, fedha za biashara, kubadilisha fedha na mwongozo wa kisheria. 

Naye Mkurugenzi wa Mahusiano ya Biashara wa Equity Group, Bw. AQ Hamza, alieleza kuwa misafara ya biashara ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi, kujenga mahusiano ya kibiashara na kuwezesha biashara za kimataifa. 

Aidha, Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Biashara wa TanTrade, Bw. Jonathan Nkwabi, aliwasilisha fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji nchini Tanzania, kabla ya wawekezaji hao kutembelea maonesho ya Sabasaba na kujionea sekta mbalimbali za biashara na uzalishaji.





















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...