Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma
Serikali imeeleza kuwa inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wanaoathiriwa na mashambulizi ya wanyamapori katika Wilaya ya Serengeti, sambamba na kuchukua hatua za kudhibiti wanyama hatari wanaotoka kwenye hifadhi na kuingia katika makazi ya watu.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Dkt. Jafar Seif akijibu swali la Mbunge wa Serengeti, Mary Daniel Surati, ambaye alitaka kufahamu mkakati wa Serikali wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wanaokumbwa na madhara ya wanyamapori.
Dkt. seif amesema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili wananchi wanaoishi au kufanya shughuli za kijamii katika maeneo yanayopakana na hifadhi zenye wanyamapori, ikiwemo Hifadhi ya Serengeti.
Amesema miongoni mwa mikakati inayotekelezwa ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga dhidi ya wanyama hatari kama tembo, simba, chui na fisi, pamoja na kuhimiza utoaji wa taarifa kwa mamlaka husika mara wanapoonekana wakitoka hifadhini na kuingia kwenye makazi ya watu.
Aidha, Serikali imeendelea kuimarisha ufuatiliaji wa wanyamapori (surveillance) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo Frankfurt Zoological Society (FZS) na Grumeti Reserves. Kupitia ushirikiano huo, wanyama wanaotoka nje ya hifadhi hufuatiliwa na kurejeshwa haraka ili kupunguza hatari kwa wananchi.
Katika kuimarisha huduma za afya, Waziri amesema Serikali inaendelea kujenga na kukarabati miundombinu ya kutolea huduma za afya, ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Serengeti, vituo vya afya na zahanati. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi wanapata huduma bora za matibabu, ikiwemo kuwahudumia waathirika wa mashambulizi ya wanyamapori kwa wakati.
Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha usalama wa wananchi unaimarishwa huku huduma za afya zikiboreshwa ili kupunguza athari zinazotokana na migongano kati ya binadamu na wanyamapori.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...