Na Mwandishi wetu, DODOMA

Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro, amesema kuwa uwekaji wa vyombo vya kuhifadhia taka katika maeneo mbalimbali ya barabara ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha usafi wa mazingira na kudhibiti utupaji holela wa taka ndani ya jiji hilo.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuweka vyombo hivyo, Kimaro alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwahamasisha wananchi kutumia maeneo rasmi ya kutupia taka na kuongeza uwajibikaji katika utunzaji wa mazingira. Alibainisha kuwa uwepo wa vyombo vya kuhifadhia taka utarahisisha ukusanyaji wa taka na kuifanya Dodoma kuwa jiji safi, salama na lenye mazingira bora kwa wakazi na wageni.

"Tunawaomba wananchi watumie vihifadhi taka hivu kwa usahihi na kuepuka kutupa taka hovyo. Ushirikiano wa jamii ni muhimu katika kuhakikisha tunadumisha usafi wa jiji letu wakati wote. Tutaimarisha ulinzi kwenye hizi barabara ili kuhakikisha vyombo hivi haviharibiwi ukizingatia tumeweka kamera za ulinzi katika barabara zetu za jiji pia kwa yeyote atayekiuka agizo sheria zitafuatwa dhidi yake" alisema Kimaro.

Aidha, alieleza kuwa mamlaka za jiji zitaendelea kuboresha huduma za usafi wa mazingira kwa kuongeza miundombinu ya kuhifadhi taka pamoja na kuimarisha elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa usafi na utunzaji wa mazingira.

Alisema vyombo hivyo si vyakuwekea taka kutoka majumbani bali ni kuwasaidia wanaopita barabani kutupa taka mfano chupa za maji na magunzi ya mahindi.

Zoezi hilo ni sehemu ya jitihada zinazoendelea za Jiji la Dodoma za kuboresha mazingira yake ili kuzuia uchafuzi wa mazingira na kulinda afya za wananchi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...